Yanga, kaeni mkijua Jumamosi lazima tugawane furaha nusu fainal ASFC

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Simba imewaudhi mashabiki zake kwa kuwadanganya kuwa raundi ya 2 watakamata usukani na kuendeleza yale ya msimu uliopita kwa kubeba ubingwa, kilichopo sasa ni dhahiri mtani amenyanyua makwapa, kuna uwezekano mkubwa kuzuka kwa mgogoro ndani ya timu.

Inaonekana watu wa mpira Simba wamepotea, akina Kassim Dewji tunaowategemea kuleta mabadiliko hawawezi tena kwenda na kasi, wamezidiwa mbinu na watoto wa mjini Yanga wakimtumia sana Albino Manara.

Njia pekee ya Simba kurudisha angalau aman ndani ya timu ni kugawana furaha na yanga hiyo jumamosi, bila hapo ni ugomvi tu kwenda mbele.
 
Tunaanzaje kugawana furaha na wasiojua mpira !? Mtapigwa kipigo cha mbwa koko...!! Na baada ya pale mtapoteana wachawi nyie
 
Simba akishinda Tarehe 28 nitaishangaa Yanga, maana kila kitu kipo kwenye Mahakama yao... Simba yenye forward isiyoeleweka, viungo wapenda kukaa na MPIRA na kupiga pasi Milioni zisizo na faida.. angalau Mabeki wanatupa moyo...
 
Tutaweza kweli?

Waamuzi wa huo mchezo tumeshawaweka sawa na baadhi ya wachezaji wa Utopolo?
 
Wanasimba tuache kujijitumua tukubali huu msimu tuliteleza .
Sioni timu ya kumtoa yanga siku ya jumamosi .
Hawa wa kina sako ,kagere ,bocco,kibu ,kanoute,bwalya ,Gadiel ndio waamue matokeo ya jumamosi?
Hapana mm ni Simba ila jumamosi Simba out na nataka iwe ivyo ili msimu ujao wasajir vzr maana walianza kubweteka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…