YANGA kamili kuifuata KAGERA SUGAR kesho

shemaghotwe

Member
Joined
Apr 14, 2014
Posts
93
Reaction score
67
Yanga inaondoka kesho asubuhi kwenda Bukoba tayari kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaofanyika Jumamosi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Yanga, Dismas Ten alisema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo akiwemo Amissi Tambwe aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu.

“Timu imefanya mazoezi jana na leo Jumanne kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ujao. Kesho timu itaondoka asubuhi kwenda Bukoba tayari kwa mchezo huo.

“Wachezaji wote wako vizuri na tunafurahi kuwa Tambwe amerejea na atakuwemo ingawa maamuzi ya kucheza au kutokucheza yatabaki kwa kocha. Pia Obrey Chirwa naye yuko fiti,” alisema Tena.

Yanga itaikabili Kagera Sugar Jumamosi huku ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 6-2 ilioupata kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Katika mchezo huo mabao ya Yanga yalifungwa na Ngoma aliyefunga mawili sawa na Chirwa huku Simon Msuva ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa nchini Morocco, alifunga moja na lingine likifungwa na Deus Kaseke ambaye kwa sasa anaichezea Singida United.

Yanga itaikabili Kagera Sugar ambayo hadi sasa ndio moja kati ya timu tatu ambazo hazijapata ushindi wowote tangu Ligi Kuu Bara ianze msimu huu. Timu nyingine ni Ruvu Shooting na Majimaji.


From Mwanaspoti
 

Attachments

  • PIC+YANGA%5C.jpg
    28.8 KB · Views: 28
Sare inawahusu
 
Sawa, wapo kamili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…