Yanga kujiita "watoto wa mama" haya ndo matunda yake

Yanga kujiita "watoto wa mama" haya ndo matunda yake

Wakipekee

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
6,194
Reaction score
10,711
Kabla ya msimu huu kuanza ingekua ngumu kuamini Yanga itakua imepoteana kiasi cha kua kama togwa la kwenye harusi Kila mtu anajichotea tu..

Kwanza pre season pale south Africa, Yanga ilionekana kua timu tishio baada ya kucheza soka la kuvutia na kupata matokeo mazuri dhidi ya Kaizer Chiefs kwa kuwapiga bao nne bila, pia licha ya kufungwa na Augsburg timu toka ligi kuu ya ujerumani kwa 2-1 lakini Yanga ilitandaza soka safi...

Yanga ilianza ligi kwa staili ambayo haikua ya kuvutia japo ilikua ikipata matokeo hadi pale ilipigwa na Azam fc, baada ya hapo graph ya Yanga ilianza kwenda chini kwa spidi ya lami na kugongwa kama kengele.

Nilikua siamini kama Yanga imeshuka kiwango ila kwa nilichokiona Jana nimekubali Yanga ni janga kwa sasa Kila mtu atajipigia vinginevyo yanahitajika mabadiliko ya fasta..

Kwa maoni yangu kosa la Yanga ni kujiita "mtoto wa mama" kuchanganya siasa na mpira kwa masilahi ya watu wachache haya ndo madhara yake. Na bado nahisi Kuna maumivu makubwa zaidi yanakuja msimu huu tutazidi kupoteana.

Goli la mama halichezi mpira acheni ujinga wenu, mbona timu ikipoteza mechi hao Wanasiasa hukaa kimya? Ila ikishinda sasa... na msimu huu tusipokua makini tutaliza namba nne....

Nini kifanyike !??? Ili watoto wa mama wasiteseke ? Itabidi tujifunze mbinu za "kushinda kwa kishindo..."
images%20(2).jpg
 
Timu alizo cheza nazo vinonde kaizer ipo nafas 9 galaxy 7 walikuwa wanacheza na kmc ya bongo kifup walipga mabomu mochwali
 
Timu alizo cheza nazo vinonde kaizer ipo nafas 9 galaxy 7 walikuwa wanacheza na kmc ya bongo kifup waliga bomu mochwali
Walau kipindi kile walicheza soka zuri sahivi wanakandwa na mpira haueleweki
 
Tanzania Bado sana Kwenye Mpira
Tumejaa Makelele ya Mdomoni na Siasa Zakipumbavu.
Unayo yaona kwa Yanga hata Simba Nivile vile
Leo hii Simba Ina Hangaika Mwaka wa 7 kufanya Mabadiliko lakini ni Serekali inayo kuwa Kikwazo kwao.
Wakishinda wanajipa Sifa wakati mambo muhimu ya Club Hawataki Kuunga mkono
 
Back
Top Bottom