Yanga kumaliza na emmen fc ya uholanzi kesho

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
[h=2]Thursday, January 10, 2013[/h][h=3][/h]


Wachezaj wa Young Africans wakifanya mazoezi leo asubuhi kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Emmen FC ya Uholanzi
Timu ya Young Africans Sports Club kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa mwisho na watatu (3) dhidi ya timu ya Emmen FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika katika viwanja vya Adora football - Berek pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.
Young Africans ambayo imeshakaa takribani siku 12 katika mji wa Antalya na kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu za Armini Bielefeld ya Ujerumani na Denizlispor ya Uturuki leo asubuhi imeendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence football mjini Antalya.


Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema atatumia mchezo huo wa mwisho kama fursa pekee kwao kwani mchezo huo utakuwa kipimo kizuri kwao kwani timu ya Emmen FC ni timu nzuri na ndio maana ipo katika ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi.


Akiongelea mchezo huo wa kesho Brandts amesema timu ya Emmen FC ni timu nzuri, imekuja Antalya kuweka kambi ya mafunzo kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi, hivyo ni nafasi nzuri ya kujipima uwezo na timu hiyo ya Uholanzi.


Aidha wachezaji Frank Domayo na Kelvin Yondani waliokuwa wameondoka jana jioni kuelekea nchini Ethiopia wameshindwa kuungana na wachezaji wenzao wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya jana jioni kufika Istambul kukuta tiketi zao za kwenda Addis Ababa ni za tarehe 09 Februari 2013 hali iliyopelekea kukwama Istambul na kuamua kurejea mjini Antalya kuungana na wachezaji wenzao waliopo kambi.


Kikosi cha wachezaji 27 waliopo kambi mjini Antalya kimeendelea na mazoezi ya asubuhi kujiandaa na mchezo huo wa kesho amabao utakua ni mchezo wa mwisho kabla ya timu ya Young Africans kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania siku ya jumapili.


Young Africans inatarajia kuondoka mjini Antalya siku ya jumapili mchana kupitia Istambul ambapo itaondoka majira ya saa 1 usiku, saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na inatarajiwa kufika Dar es salaam Tanzania majira ya saa 10 usiku kasoro.

Jerson Tegete, Omega Seme & Ladislaus Mobgo wakiwa mazoezini leo asubuhi


at 7:26 AM



 
Haya HADI GLOVE's ?? Safi...
 
Nawatakia kila la kheri vijana
 
Timu makini yenye wanachama makini. Wapi Ragee!!!
 
Simba Daima Nyuma, Kwenda Mbele Mwiko.
 
Halafu bonge la promo. Siku watakaporudi na kuwa na mechi taifa itakuwa nyomi kinoma! Nani atakaa nyumbani asiende kuona chama la ukweli?

Sent from my GT-P7500 using Tapatalk 2
 
Mbona sioni picha za mtaani akiwa eapoti au ndo kaenda natreni ya mwakyembe.
Naitaji nione hata kagest walikofikia apo oman isje kua wamefikia kwa yule mama alietoa tiket hizo30. Wengine wanalala sebreni wengine stoo make rage haaminiki kabisa
 
Haya HADI GLOVE's ?? Safi...
Yeah, kuna mtu humu alisema wanafanya mazoezi kwenye nchi ya baridi kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayochezwa nchi yenye joto! Yanga bana!
 
Yeah, kuna mtu humu alisema wanafanya mazoezi kwenye nchi ya baridi kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayochezwa nchi yenye joto! Yanga bana!

nawaonaga man u wakiweka kambi qatar na nchi nyingine za kiarabu kwani huko lini kunakuaga na barid kama la wingereza,??
 
Yeah, kuna mtu humu alisema wanafanya mazoezi kwenye nchi ya baridi kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayochezwa nchi yenye joto! Yanga bana!



Unajua ni VIZURI kufanya MAZOEZI kwenye HIGHER ALTITUDE inapanua MAPAFU... na kama UKIIZOEA hali hiyo - MPIRANI hautachoka.

TURKEY sio BARIDI ila sehemu waliyoweka KAMBI iko JUU KIDOGO ya USAWA wa BAHARI...

HII ITAKUA ADVANTAGE NZURI kweli kwa Wachezaji wa YANGA; zaidi ya SIMBA kwenda NCHI ya jOTO zaidi ya BONGO
 
mechi pili yanga ilicheza na nani na matokeo yalikuwaje huko turkey?
 
simba wana tamaa ya fisi. eti wengine wapo zanziba na wengine wameenda uarabuni na wengine wamebaki dar. hawaeleweki yaani moja hawakai mbili hawakai. mia
 
Chama laukweli Azam tu wengine siasa zime wajaa
 
Hili ndo Chama la kushabikia,mtu unakuwa proud nalo!
 
Yeah, kuna mtu humu alisema wanafanya mazoezi kwenye nchi ya baridi kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayochezwa nchi yenye joto! Yanga bana!

Dah kweli elimu uliyoipata haijakuwa msaada kwako...yote tu hiyo ni kuongea kishabiki ili upigiwe makofi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…