Yanga kupeleka msiba kwa Sagrada mjini Dundo leo

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
338
Reaction score
180

MABINGWA wa soka Tanzania, Yanga, leo wanajitupa kwenye Uwanja wa Estádio Sagrada Esperança mjini Dundo mbele ya watazamaji 8,000 kupambana na wenyeji GD Sagrada, katika mechi ambayo inaweza kuwaacha wenyeji wakiwa kwenye msiba mzito.

Yanga inahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili iweze kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wake wa mabao 2-0 ilioupata jijini Dar es Salaam katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu.

Wachezaji raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoku ambao walikosa mechi ya kwanza, leo watakuwa uwanjani kuongeza nguvu ili kuihakikishia timu hiyo ushindi muhimu na kufuzu kwa hatua hiyo adhimu.

Soma zaidi hapa => http://www.fikrapevu.com/yanga-kupeleka-msiba-kwa-sagrada-mjini-dundo-leo/
 
Leo fanza mambo Angola.... Yangaaa.........
 
Daima mbele nyuma mwiko,chura viroho vinawauma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…