Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258
Yanga inakabiliwa na faini ya Sh milioni 128 kwa uzembe wa kuchelewa kufanya usajili wake kwenye mtandao wa kimataifa (TMS). Yanga ambayo tayari utetezi wake umetua Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), iwapo utakubaliwa klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani italazimika kumlipia kila mchezaji dola za Marekani 500 na klabu hiyo ina wachezaji 27 ambao italazimika kuwalipia dola za Marekani 13500 (sawa na Sh milioni 128).