Yanga kutumia kikosi hiki naamini tunaweza kupata matokeo

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
~ 1 Diarra

~ 2 DJUMA

~ 4 JOB

~ 5 Nondo

~ 6 Joyce

~ 6 Bangala

~ 7 Fei

~ 8 Aucho

~ 11 Benard

~ 9 MAYELE

~ 10 Makambo

Kwanini hivi naamini kikosi hiki kinaweza kuleta ushindi, kwa maana hawa mabwana watazuia sana nyuma kwa hiyo itabidi wachezaji wetu wa pembeni wawe wanapiga ile mipira ya juu kutafuta washambuliaji, na kwenye mipira ya juu wote mnajua Makambo vizuri kwa vichwa. Na mayele naye kidogo.

Na pia sister hii itakuwa inampa Djuma nafasi ya kupanda maana akipanda Fei ana shuka na Fei kukaba anaweza.
 
Sasa hivi Yanga wanaandika nyuzi zao kwa weledi bila kumdharau mpinzani, wiki moja iliyopita walikua wanaishi ulimwengu wa kipekee. Kila timu walikua wanajua itakua Zalan FC.

Al Hilal asanteni kwa kuwarejesha watu katika default setting.
 
Wale jamaa kwa mipira ya juu mtapigwa kama ngoma
 
Kwisha hongera aseeh unajitahidi na manyuzi ya Yanga
 
Naona umepanga kikosi ukiamini Hilal watakuwa wanawasubiri tu golini kwao ndio wawazuie.
1. Diarra ni very shaky akiwa golini. Mechi iliyopita aliokolewa na beki na papara ya wachezaji wa Hilal.
2. Kile kikosi cha Hilal kilichocheza kilikuwa na idadi kubwa ya mabeki na viungo wakabaji ila walikuwa na on target 6. Mechi ya kesho watachezesha mawinga na viungo washambuliaji zaidi.
3. Lomalisa ni beki asiyejiamini, anapiga back pasi nyingi kama mkude wa Simba.
4. Morrison na makambo hawasaidii timu kukaba inaposhambuliwa na Fei akikaba lazima iwe faulo.
5. Wasudan wanajua kutoa mpinzani mchezoni na hivyo Aucho, Djuma au Diarra au bangala wana hatari ya mmoja au wawili kula umeme.
6. Mwapunyeto wote tunajua uwezo wake.
7. Nabi huwa hana plan b ya kikosi. Kikosi atakachoanza nacho ndio huwa kamaliza top layer yote.
 

Ulikuja na utabiri wako uchwara hapa, baada ya mechi ni kubwabwaja tu!
Utopolo mnatabu sana, jipeni moyo tu eti mnaenda kushinda Pale Khartom!
 
Hahahaaa namba 3 hakuna. Mmeanza kudata kabla ya mechi.
 
Yanga zake mechi za mchangani, kimataifa amwachie Simba
Sikio haliwezi kuzidi kichwa hata siku mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…