HPAUL
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 410
- 567
Hayo ni maneno ya Haji Manara
YANGA KUUKOSA UBINGWA WA LIGI KUU BARA KWA MISIMU 10 IJAYO - SALEH JEMBE
YANGA KUUKOSA UBINGWA WA LIGI KUU BARA KWA MISIMU 10 IJAYO - SALEH JEMBE
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yule tutamshitaki kwa vitendo Mtani kuonyesha kwamba kazungumza kwa mihemko na si uhalisia wa mambo.Yanga wakamshitaki Haji mahakamani kwa defamation,haaaaa haaaa
Mtani 100 Likes nimekutana na hii mpya huku. Aiseee
Hajielewi yule.Mimi ni mshabiki wa Simba lakini Haji simchukulii kama msemaji wa Simba.
Yule anatakiwa awe kwenye kitengo cha ngoma na uhamasishaji, especially kwa sasa tunapotaka timu ifanye kazi at corporate level.
Ninatarajia kwamba msimu ujao tutakuwa na msemaji, na Haji atapewa kitengo chake cha propaganda.
Hajielewi yule.
Ila si ndiyo maneno washabiki wanataka kuyasikia?
Maana nakumbuka nyie mliwahi kuwa na Muro, tabu tupu ilikuwa.
Hahaaa. Na kweli Mtani ndio tunavyopenda hivyo yaani hapo kila sifa atapewa na Mashabiki wake kwa kuwa kaona mbali. Teh.
Hahaa. Yule Muro naye si sawa na Manara tu na ndio sababu wanaiva chungu kimoja.
Yaani jamaa hao mahali serious wanashusha pumba, hawawezi kuzungumza kitu ukakitilia maanani.
Na raha yao ni kukarahisha watu.
Ila tusubiri hiyo Miaka kumi aliyoisema Manara Mtani huenda.
Hayo maneno ya kishabiki tu, sidhani kama aliyaongea akiwa serious.
Maana hata siku ile akisema Barcelona anakufa kwa Mchina.
Na itakuwa yamechagizwa na uwepo wa Mo kwa kipindi chote hicho.
Si Mo yupo Simba kwa miaka 10 au mi ndio nimechanganya mafile?
Mo yupo simba kipindi chote cha maisha yake labda apate uamuzi wa kumuudhia mtu mwingine hisa zake za asilimia 49% alizowekeza kwenye club. Kwaiyo hata akifa kesho asilimia 49 ya simba ni sehemu kampuni yake, hivyo itaendelezwa na familia. Kwaiyo akina akilimali wakiendelea ng'ang'ania mna miaka mingi ya maumivu kama sisi mashabiki wa arsenal tunavyouguliagaNa itakuwa yamechagizwa na uwepo wa Mo kwa kipindi chote hicho.
Si Mo yupo Simba kwa miaka 10 au mi ndio nimechanganya mafile?
Yes, Simba wanaye Mo.
Je Yanga hawatapata mtu?
Maana kitu kizuri ni kujifunza kwa mwenzio, kadri Simba atakavyopata mafanikio kutokana na mfumo huo Yanga hawatakuwa na budi kutoiga, na wakishaiga unategemea Simba aendelee kushinda tu?
Ndio hapo sasa.
Na hiki ulichokiandika ndio Manara hajakiwaza sasa sababu hata mi naamini tupo katika hali ya Mpito na sio kwamba tutakuwa hivi maisha yote.
Mo yupo simba kipindi chote cha maisha yake labda apate uamuzi wa kumuudhia mtu mwingine hisa zake za asilimia 49% alizowekeza kwenye club. Kwaiyo hata akifa kesho asilimia 49 ya simba ni sehemu kampuni yake, hivyo itaendelezwa na familia. Kwaiyo akina akilimali wakiendelea ng'ang'ania mna miaka mingi ya maumivu kama sisi mashabiki wa arsenal tunavyouguliaga