kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Nembo ya Vodacom ina wekundu na weusi kitu kinachowapa kigugumizi wenzangu wa Yanga kuweza kuivaa kwenye jezi zao kama ilivyo eti kuepuka lile doa nyekundu kwenye nembo. Miaka iliyopita walilazimisha nembo hiyo kubadilishwa rangi na kuwa nyeusi. Hii nadhani sio Sawa Kwa wenzangu wa Yanga kwakuwa rangi nyekundu sio ya Simba na ilikuwepo hata kabla ya Simba kuanzishishwa. Damu zetu ni nyekundu, sare za wanajeshi zina wekundu, nishani zina wekundu, mapapai yako mekundu, madaladala yako yenye rangi nyekundu na nyama ni nyekundu. Kuvaa nembo Tu hakutoshi kuinajisi jezi yote kuwa haifai kwasababu kinembo cha Vodacom kina wekundu.
Hela ya mdhamini tunataka lakini nembo yake hatuitaki. Tuache ukorofi na ushamba kwenye hela za watu.
Hela ya mdhamini tunataka lakini nembo yake hatuitaki. Tuache ukorofi na ushamba kwenye hela za watu.