sos_10
Member
- Jun 23, 2024
- 7
- 21
Kauli iliyotolewa na afisa habari wa Yanga bw Ally Kamwe kwa kuwaita wa ovyo watu waliotinga mahakamani kupinga uhalali wa uongozi wa Yanga na kupewa ushindi ni kuidharau Mahakama iliyotoa hukumu na kuwapa ushindi watu hao baada ya kusikiliza madai yao na kuona yana mashiko.
Nadhani ule muda waliotumia kuita vyombo vya habari kuwakandia na kuwabeza watu hao wangeutumia kujipanga na mwanasheria wao ili kwenda kupambana kisheria na watu hao wawili wanaowaumuiza vichwa.
Lakini pia inafikirisha kauli iliyotolewa na mwanasheria wa Yanga kuwa wakati kesi ikiendelea mahakamani na mpaka hukumu inatoka uongozi wa Yanga haukuwa na taarifa.
Sidhani kama Mahakama inaweza kuendesha kesi kwa kusikiliza upande mmoja, yaani kusikiliza upande wa Mdai bila ya Mdaiwa kupewa nafasi ya kujitetea.