Yanga Kuweni Makini na Ahadi Zenu kwa Wachezaji

Matungiza

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2017
Posts
523
Reaction score
335
Klabu ya Yanga inadaiwa kiasi kikubwa na wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu. Wachezaji hao inasemekana waliahidiwa kumaliziwa chao katika mechi za awali katika mzunguko wa kwanza.

Wachezaji hao walipotaka kupata ufafanuzi kwanini ahadi zao hazitekelezwi, inasemekana uongozi ulitaka kuwatisha ili wasisungumzie suala hili hadi wakati wa mapumziko ya baada ya ngwe ya kwanza.

Baadhi ya wachezaji ambao hawakutaka majina yao kutajwa walisikika wakilaumu na kusema mpira ni kazi yetu, kutishana ni zilipendwa, sisi tunadai chetu.

Unajua uongozi unawathamini sana wachezaji kutoka nje, madai yao wanatekelezewa haraka.

Yanga huu siyo wakati wa kubishana na wachezaji.
 
Suala la kuthamini zaid wachezaji kutoka nje bila kujali mchango wao katika timu ni kubwa mno hata simba litakuja kuwaletea shida mbeleni. Angalia kiwango cha mavugo vs wachezaji wa ndani halafu fuatilia mshahara wake utajua kua kuna tatizo kubwa litakuja kutokea mbelen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…