Yanga, mfanyieni hivi Mrisho Ngassa, mtapata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Mrisho Ngassa Ni mchezaji aliyeichezea klabu ya Yanga kwa mapenzi makubwa mno.

Ameitumikia Yanga kwa uaminifu mkubwa mno na kwa nguvu zake zote, akili zake zote na kwa moyo wake wote.

Mrisho Ngassa aliwahi kukataa ofa ya billion moja kwenda Sudan ili tu abaki na Yanga yake.

Kwa hayo machache aliyoifanyia Yanga, Ingependeza zaidi Yanga imuandalie Mrisho Ngassa mechi ya kumuaga kwa heshima, kisha abebwe kwenye kiti kifalme ili kuthamini mchango wake kwa Club.

Pia itakuwa ni heshima kubwa kwa club ya Yanga iwapo itaitenga namba ya jezi ya Mrisho Ngassa Kama kuienzi na kuheshimu mchango wa legendary huyo barobaro.
 
Utopolo makaidi SANA ushauri Kama huu kwao hauthaminiki
 
Mussa Mgosi anaenjoy tu msimbazi
Nguvu moja
 
Hivi vyote havitasolve njaa aliyonayo sasa
 
Ngasa alizingua kusema kweli, nadhani hakupata watu wa kumshauri.
Kumshaurinini sasa wakati lilikua lishakua jituzima na linaakili zaketimamu.na alishauriwa maranyingi achukue dau la pesandefu za wasudani zaidi ya b 1.
 
Za kuambiwa tuchanganye na zetu...Ngasa hana jeuri ya kukataa Bilioni moja...Hivi Bilioni moja mnaijua mnaisikia? Huyo Makusu Mundele kanunuliwa kwa Bilioni moja na ushehe miaka hii ya karibuni...Huyo Ngasa hana guts za kukataa Bilioni moja ni sifa za kijinga tulizopeana bongo tukishirikiana na Magazeti ya michezo ambayo ni kama udaku tu...miaka ile

Eti Bilioni moja! Seriously?
 
Mashabiki wa simba ni sawa na wanawake waimba taarabu
 
Mrisho Ngassa aliwahi kukataa ofa ya billion moja kwenda Sudan ili tu abaki na Yanga yake.
Pia alikubali kulipa faini ya sh. milioni 15 pamoja na kurudisha sh. milioni 30 alizokuwa tayari ameshazitumia (jumla alilipa milioni 45) ili afanikishe kuhamia Yanga kutoka Simba iliyokuwa imemsainisha mkataba wa miaka miwili zaidi mbele ya mwaka mmoja wa mkopo kutoka Azam
 
Ngasa angepunguza mikogo apate kula Vancouver
 
Hivi vyote havitasolve njaa aliyonayo sasa
Niliwahi mkuta mtwara akiwa na ndanda fc...aseee huyu jamaa ni moja ya wajinga sana. Alikuwa na amafanikio tele akayachezea.

Acha apambane na hali yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…