Yanga mkienda na takwimu hizi kule kwao mtatoka matokeo

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Namba 1 - Mshery

Walinzi
  • Job
  • Bangala
  • Baka

Katikati
  • Fei toto
  • Aucho
  • Zawadi mauya
  • Djuma Shaban
  • Lomalisa

Mbele
  • Mayele
  • Makambo

Kwanini nimeweka katikati wachezaji wa 5? Kwasababu kule kwao Al Hilal hawatotafuta ushindi sana, bali watalazimisha sare, kwa hiyo watacheza mpira wa kuzuia na kufanya mashambulizi ya kustukiza.

Kwa hiyo basi Yanga wanatakiwa wacheze mchezo wa kushambulia, mpira wa kuzalisha sana mashuti katikati ya uwanja kuliko kutafuta namba 9.

Huu ndiyo mpira ambao Yanga wanatakiwa wacheze. Itakuwa hivi;

Job atacheza kama DCG, yaani atakuwa anachezea pembeni kama namba 2 na 5, huku Bangala atacheza kama DCD yaani atakuwa anacheza kama na 3 na 4.

Huku Aucho na Mauya watacheza kama MCD, yaani watakuwa wanacheza kama namba 6 na 5 timu inaposhambulia ili kuziba pengo katikati.

Djuma ana cheza kama namba MG kwa ufupi ni kama namba 7 ya mchongo, na Nalomalisa anacheza kama MD. Na hii namba 11 ya mchongo watakuwa wanapanda timu inaposhambulio na kushuka timu inapo jilinda kuja kukabia katikati.

Huku Fei na Aziz Ki watacheza kama namba 10 na 8, kushambulia kwa kupiga mashuti ya kati.
 
Nani kakudanganya Al Hilal watacheza mpira wa sare?

We kama ni kocha ukisikika hivyo kwa waajiri wako utapigwa na vibao

Halafu pamoja na juhudi zote alizofanya Diarra leo hadi kuibuka man of the match lakini katika kikosi chako ulichokipendekeza hayupo festi ileveni?

Huyo Makambo impact yake ni kwenye mechi za mikoani huko, huko mara nyingi namuona ana ng'aa zaidi kumzidi hadi Mayele lakini sio huku unakotaka kumuweka.

Kuwajaza mbele wote kwa pamoja hakutaweza kuwasaidia kupata matokeo labda kama Mohamed Abdelrahman Yousif Yagoub siku hiyo hata cheza

Halafu ulivyokosa busara na Kisinda naye hujamuweka, nyie si mlimsajili kwasababu ya mikimbio?

Mshangundua mwana talent yake ilikuwa ni marathon na sio soccer?
 
uyo baka kwenye defenceve ni baka wa wapi?
 
Ibenge wakati anasaini Al hilaly aliambiwa akishindwa kuingia makundi kazi hana.

kwa unavyomjua Ibenge kocha bora baada ya Mosemane anaweza kweli kukosa kuingia makundi?
 
Huyo KI atacheza vipi kwenye kikosi hayupo kuwa serious na tu vitu vitu utaenda mbali
 
Leo timu yenu inacheza! Mhamie huko sasa kuchambua. Na kiukweli nitafurahia sana iwapo itafungwa, ili akili zenu ziwakae sawa.

By the way, kufungwa hakumwepeki. Na mwezi huu utakuwa ni wa mateso makubwa kwenu. Maana kuna hao Waangola, kuna Wananchi, na mtamalizia na Azam.
 
We mzee una matatizo
 
We mzee una matatizo
Muanzishe sasa nyuzi za kuijadili timu yenu! Inacheza leo na Waangola. Ma huenda ikapoteza ugenini.

Yanga imeshacheza! Na imeendeleza wimbi lake la kutopoteza katika mechi za kiushindani, ndani na nje ya nchi!
 
April targets za ssc ni kuchukua point 12 za ligi na kutinga makundi championship. Nyie zenu ni zipi au mnaenda enda tu kama upepo?
 
Sio tuwapige Waangola kisha uje kusema ni vibonde.
 
Sio tuwapige Waangola kisha uje kusema ni vibonde.
Timu inayotolewa kamasi na KMC ndiyo iwafunge Waangola! Labda kama hao Waangola wako level za akina Nyasa Big Bullets.

Kinyume na hapo, nakuhakikishia simba ya msimu huu ni ya kawaida sana. Na hata hizi mechi mbili tatu ilizoshinda, zimechangiwa na hanasa tu ya Kocha Juma Mgunda! Nothing more.
 
April targets za ssc ni kuchukua point 12 za ligi na kutinga makundi championship. Nyie zenu ni zipi au mnaenda enda tu kama upepo?
Mna target ipi nyinyi! Timu kwa sasa inacheza kwa hamasa ya kocha Juma Mgunda!

Halafu hizo April targets sijui ni zipi! Maana tuko mwezi Oktoba sasa! Mwezi ambao mtafungwa na kupoteana sana tu!
 
Hakuna kipa wa kumweka nje diarra wewe Acha na huyo mtoto mjinga mjinga atafungwa goli kumi
 
Muanzishe sasa nyuzi za kuijadili timu yenu! Inacheza leo na Waangola. Ma huenda ikapoteza ugenini.

Yanga imeshacheza! Na imeendeleza wimbi lake la kutopoteza katika mechi za kiushindani, ndani na nje ya nchi!
Usitupangie cha kupost humu,ukiona post haiko mrengo wako ikaushie tu la sivyo utapata wazimu bure kukoromeana na kila anayeisema Yanga yako.
 
Al hilal hawezi kuizuia Yanga kutinga Makundi.
Umeota ndoto hii ukiwa wapi!
Unateseka ukiwa umekaa wapi ndugu utopolo! Nyie endeleeni kutetema humu humu ndani. Huko nje waachieni wenye sharubu zao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…