Naamini uliingalia mechi, dakika chache sana kipindi cha mwisho club africain walitoa intro tu ya uchezaji wao na kilichotokea yanga walichanganyikiwa, mechi ya marudiano itakuwa dhahama kubwa kwa yanga.
Ushauri
Acheni zile kebehi zenu mcheze mpira, mlianza na al hilal mkasema hawana timu mara mmewekeza zaid yao kilichofuata ni nyie kuhamishiwa kwenye kombe la loosers kwa mujibu wa manara.
Huku kwa loosers nako mlitahadharishwa muache ngebe mkasema club africain hata haijulikan eti ndo mmeisikia na ni timu mdogo tu hivyo haiwez kuizuia, kilichotokea mech ya dar kimeonesha nan mkubwa, mmojq alicheza kwa uwezo wake wotewingine aliamua kurelax ili adroo
Points of discussion kwa wanayanga wote
1. Club africain walifikaje hapa mpaka wanakutana na yanga?
2. Club africain ina wachezaji wenye profile zipi mpaka waiwakilishe tunisia kisoka kwenye ngaz ya clun?
3. Uwekezaji wa yanga na club africain upi mkubwa ukizingatia yanga ana GSM na club africain wana Qatar airways?
Maswali haya ilitakiwa viongoz wa yanga wawe washayajibu kabla ya mechi ya dar