Yanga na rangi Nyekundu kwenye Logo ya NBC Bank

Yanga na rangi Nyekundu kwenye Logo ya NBC Bank

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mapema leo, NBC Bank na TFF zimeingia ubia wa udhamini wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, NBC wakiweka mezani bilioni 7.5 kwa kipindi cha miaka 3.

Moja kati ya faida anazotarajiwa kupata NBC Bank kama mdhamini ni uwepo wa nembo/chapa yake (Logo Placement), katika jezi za timu shiriki katika Ligi Kuu.

Nembo rasmi ya NBC ina Twiga pamoja na Mlima Kilimanjaro, lakini kimbembe ni kwamba Twiga aliyepo kwenye nembo hiyo ana rangi nyekundu, rangi ambayo pia ipo kwenye logo ya Vodacom.

Rangi hii ndio ambayo mabingwa wa kihistoria Dar Young Africa waligoma isiwepo katika jezi zao. Swali hapa ni je, nini kitatokea kwa rangi ya mdhamini katika jezi watakazovaa wananchi.

MUDA UTATUPA MAJIBU, TUSUBIRI TUONE.

NBC.png
 
Shida ni nyekundu tuu au na nyeupe? Maana utopolo kuwaelewa sometime ni kazi kwelikweli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huu mjadala mbona tayari umeisha wakuu

Yule Twiga hakuna namna inabidi awe Mweusi, na ule mlima Kilimanjaro utapambwa kwa nakshi za kijani
 
Back
Top Bottom