Yanga na Simba nani anamfuata mwenzake..?

Huja

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2021
Posts
1,167
Reaction score
1,848
Nimewaza baadhi ya matukio kati ya simba na Yanga katika kuwafurahisha washabiki wake .

Nani kati Simba na yanga
nga ni timu ya matukio .. anayefanya matukio ya kumkomoa mwenzake zaidi ili awafurahishe wapenzi..
Nani anafikri ideas , nani anazifuata haya kama ni kwa mtindo mwingine..
Yupi anaweza kuumiza kichwa, yupi anaweza zaidi utani wa Jadi ili atengenze headline, vijiwe nk ..viiongozi wa taasisi wa kutafuta MEDIA attention....

Simba alipomtaja PHIRI , yanga nao pia eti wakamtaka,.... simba ilipomtaka Aziz KI yanga pia wakamtaka.
Manara alipoondoka simba ....Yanga wakamchukua.

Senzo alipondoka simba , Yanga wakamchukua...
Morrison naye Yanga wakamchukua...

Simba ilipoanza mabadiliko ( transformation ) Yanga nao wakaanza....

Simba ilipoanza SIMBA DAY , Yanga nao wakaanzisha week ya wananchi....

Simba walipotaka kumrudisha Clotous Chama, ..eti YANGA nao wakaingia vitani....

Hii inakupa taswira gani..?
 
Morrison mlimuiba wap Aziz k mliifata Yanga Yanga ndo ya kwanza kutangaza kwamba inamtaka aAziz k sasa wewe hii umeitoa wapi ndugu yetu ngoja na waja wwngone wataongezea
 
NIKIMUONA MTU ANAYACHUKULIA UZITO MAMBO YA KITANZANIA HUWA NAMWONA AKILI ZAKE HAZIKO SAWA. KAMA TAIFA HAKUNA TUWEZALO. YASIYOWEZEKANA DUNIANI HUWEZEKANA TANZANIA TU.
 
Yooote Wanaweza kukubishia Lakini La 'Yanga dei' hawachomoi...!

Wamevumilia weeee Kwa Miaka 12 huku Wakibeza 'Simba Dei' ....! Mwishoooni wakang'amua hapa Simba na Mzee Dalali wametupiga Bao hakuna budi KUIGA.....!Ndo hii Yanga Dei unaiona Sasa...!
Na ambayo Zanaco Mwaka jana Na Vipers mwaka huu Wamekuja kuchana Bikra Ya Siku Ya Wananchi Mapemaaa kabla hawajaitwa wakongwe kwenye matamasha Ya Wiki Yao.
Yangaaaaa BYUTI BYUTI....!
 
Morrison simba ndiyo walimleta bongo.

Tukisema wewe ni tahira tunakuonea sana.
 
NB:yanga wenye akili ni kikwete na baba yake manara tu wengine wote kwa udhamini wa lucy aymel.
 
Hahahaaa!! Goodnight!
 
Yanga ndio timu kubwa. Kila mwaka inaishia makundi ya mechi za CAF.

Msimu huu wanaenda kuchukua kombe la Club Bingwa Afrika.

Mbele daima. Nyuma ni mwiko [emoji102]
 
Simba wameiiga Yanga kuanzisha timu ya mpira,Yanga imezaliwa 1935 baada ya hapo Simba nao wakaiga wakaanzisha timu yao.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
1)Mwaka 1977, Simba iliweka rekodi katika mechi za watani wa jadi kwa kuifunga Yanga mabao 6-0.

Zaidi ya miaka 42 rekodi hiyo haijafikiwa.
2)Mwaka 1938, Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikuwa timu ya kwanza kucheza na jezi,
Tukio hilo lilitokea ilipocheza na timu ya kombaini ya mabaharia wa meli zinazotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.

3)Mwaka 1941, (Sunderland) kwa sasa Simba SC ilikuwa timu ya kwanza nchini kuvaa viatu,
Tukio hilo lilitokea kwenye mechi rasmi ya mashindano dhidi ya timu ya jeshi la maji la mkoloni la Afrika Mashariki.

4)Mwaka 1959, kabla ya uhuru wa Tanganyika, kipindi hicho ikiitwa Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikwenda Ethiopia na ikawa timu ya kwanza kutoka nchini kupanda ndege.
Simba ilikwenda kwa mwaliko wa Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia.

5)Mwaka 1965, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania.

6)Mwaka 1968, Simba ilikuwa timu ya kwanza nchini kumiliki basi lake.

7)Mwaka 1974, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kuwa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati.
Pia mwaka huo Simba ikawa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufika nusu fainali ya Klabu Bingwa ya Afrika.

8)Mwaka 1979, Simba ilikuwa klabu ya kwanza na ya pekee duniani kwenye mashindano ya mabara tofauti kufungwa nyumbani magoli 4-0 na kushinda ugenini magoli 5-0 (dhidi ya Mufulira Wanderers).

9)Mwaka 1993, Simba ilikuwa klabu pekee nchini kuwahi kufika fainali ya mashindano yanayoandaliwa na CAF (kwa sasa Kombe la Shirikisho) na kucheza fainali na klabu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.

10)Simba ndio klabu inayoongoza kuchukua Kombe la Afrika Mashariki na Kati mara nyingi zaidi (makombe 6).

11)Mwaka 2003, Simba ilivunja rekodi ya Zamalek ya Misri kwa kuitoa kwenye Ligi Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya makundi.
Zamalek walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

12)Simba ndio klabu yenye makombe mengi ya jumla kuliko klabu yoyote Afrika Mashariki,
Ikiwa na vikombe rasmi vya kimashindano 58.
Hakuna klabu yoyote zaidi ya simba yenye mataji rasmi 58 kwenye nchi za Afrika Mashariki.

13)Kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Simba ndio klabu pekee ambayo kurasa zake zote za mitandao ya kijamii zimethibitishwa (verified),
Pia ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafuasi zaidi ya (followers) 2.2M.
 
Kama vile nawaona YANGA , wakitamani kuiga ....WAZEE wa kudesa ideas za SIMBA..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…