myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 166,767
- 705,461
Hivi kwanini Yanga hakushinda mechi zake zote!Mnachoteseka ni nini? Inamana Yanga ndy angetakiwa achukue? Shida mnataka bingwa awe wa upande mmoja tuu!! Kwa jins hiyo, ligi haiwezi kukua hata iweje!! Ni kama vile Yanga mnaumia sana
Kumbe hilo nalo linawaumiza? Kwa taarifa yako, mchezaji yeyote akiwa nje ya pitch, huyo refa wala hashughuliki naye, maana inawezekana ni wa akiba alikuwa anapasha! Ni ushamba tu wa golikipa na wanaomuunga mkono kama wewe! Ukitaka mchezo usimamishwe, umia ukiwa ndani ya pitch, ukiwa nje maana yake hauzuii mchezo kuendelea!kwa ufatiliaji wako wa soka umewahi sikia timu ina viporo 12
ama mpira kuendelea ikiwa golikipa kaumia
Mkuu, hebu kuwa fair kidogo basi. Kwa maandalizi yalivyokuwa (kuanzia usajili hadi kambi ya pre-season), hivi kweli Simba haikutarajiwa kubeba ubingwa? Ni timu gani unadhani ilitarajiwa ukiondoa Simba?Yanga hii ambayo kocha wake alikiri kabisa kwamba wakikutana na Simba, njia rahisi ya kuzuia magoli ni kupaki bus? Wakati mwingine muwe mnaangalia mizani basi, daah!
mihemko ya nini mkuu??Ushabiki tuweke kando, ligi yetu ya Tanzania bara ipo corrupted, kuanzia daraja la kwanza ndiyo madudu kabisa, ligi kuu bingwa anaandaliwa kabla ligi kuchezwa
Tatizo lipo TFF, nachelea kusema bodi ya ligi au chama cha marefa....sababu TFF wanajua kabisa madudu ya hizi idara na wana mandate ya kuzivunja wapo kimya.
Ushauri wangu kama hakutatokea mabadiliko kwenye hizo sehemu hapo juu...tutegemee simba kuchukua ubingwa misimu yote mpaka mabadiliko ya uongozi wa TFF, chama cha waamuzi na bodi ya ligi vipo corrupted.
ivi ukishinda mechi zako zote, viporo vya mwingine... vinakuzuiaje kuwa bingwa?kwa ufatiliaji wako wa soka umewahi sikia timu ina viporo 12
ama timu kucheza kila baada ya siku 2
ama backpass kuwa offside
ama mpira kuendelea ikiwa golikipa kaumia
kufungwa siyo tatizo, tatizo je ulifungwa kihalali....kuna figisu za kupangiwa matches za mbali mfululizo..mfano Tanga to singida then Tanga tena ukitoka hapo Lindi...makusudi tu..magoli halali kukataliwa...kunyimwa penalt za wazi nk
Kama hamkufungwa kihalali kwa nini msikate rufaa? Tena rufaa mngepeleka fifa kabisa maana tff imejaa wanasimba!
...vile vile vipi kuhusu FA, mlivyofungwa na lipuli haikuwa halali?
Kumbuka lipuli waliwafunga kwenye ligi pia!
Mkuu, Simba imecheza Dar na Ndanda siku ya Jumapili, ikasafiri kwenda Singida kucheza na Singida United keshokutwa yake siku ya Jumanne, imerudi Dar kuja kucheza na Sevilla leo Alhamis, inatakiwa icheze na Biashara keshokutwa Jumamosi. Yaani hicho ni kipande kidogo tu. Sasa wewe unalalamika Tanga-Singida-Tanga wakati kulikuwa kuna interval ya siku kibao hapo katikati?kufungwa siyo tatizo, tatizo je ulifungwa kihalali....kuna figisu za kupangiwa matches za mbali mfululizo..mfano Tanga to singida then Tanga tena ukitoka hapo Lindi...makusudi tu..magoli halali kukataliwa...kunyimwa penalt za wazi nk
mkuu unacheza match Tanga vs coast unaenda singida..ndan ya siku 2 unarudishwa tena Tanga...kwanin usipangiwe games zote za Tanga umalize then ndiyo uende singida...huoni uhuni huoMkuu, Simba imecheza Dar na Mtibwa Sugar siku ya Jumapili, ikasafiri kwenda Singida kucheza na Singida United keshokutwa yake siku ya Jumanne, imerudi Dar kuja kucheza na Sevilla leo Alhamis, inatakiwa icheze na Biashara keshokutwa Jumamosi. Yaani hicho ni kipande kidogo tu. Sasa wewe unalalamika Tanga-Singida-Tanga wakati kulikuwa kuna interval ya siku kibao hapo katikati?
Wewe unaiangalia Yanga tu, yaani hutaki hata kuangalia hizo timu za Tanga (JKT Tanzania na Coastal Union) zilikuwa ziko wapi wakati huo. Yaani unachukulia kwamba JKT na Coast zilikuwapo tu zimekaa Tanga zinaichora Yanga ikizurura!mkuu unacheza match Tanga vs coast unaenda singida..ndan ya siku 2 unarudishwa tena Tanga...kwanin usipangiwe games zote za Tanga umalize then ndiyo uende singida...huoni uhuni huo
[emoji23][emoji23][emoji23]asee mkuu..kwa ufatiliaji wako wa soka umewahi sikia timu ina viporo 12
ama timu kucheza kila baada ya siku 2
ama backpass kuwa offside
ama mpira kuendelea ikiwa golikipa kaumia
Njevya mstari una maana gani mkuuUnazijua sheria za mpira vizuri? Fuatilia kuhusiana na kipa kuumia halafu yupo nje ya mstari nini kinatakiwa kufanyika?
Unaeleza kwa hisia,uhalisia,ndoto,mihemuko,jotoridi,jakamoyo,inda,huzuni au manung'uniko?Ushabiki tuweke kando, ligi yetu ya Tanzania bara ipo corrupted, kuanzia daraja la kwanza ndiyo madudu kabisa, ligi kuu bingwa anaandaliwa kabla ligi kuchezwa
Tatizo lipo TFF, nachelea kusema bodi ya ligi au chama cha marefa....sababu TFF wanajua kabisa madudu ya hizi idara na wana mandate ya kuzivunja wapo kimya.
Ushauri wangu kama hakutatokea mabadiliko kwenye hizo sehemu hapo juu...tutegemee simba kuchukua ubingwa misimu yote mpaka mabadiliko ya uongozi wa TFF, chama cha waamuzi na bodi ya ligi vipo corrupted.
Kwahiyo kuhusu viporo ulitaka simba wanyanganywe asicheze au? Maana walikuwa wanacheza kimataifa hakukua na namna nyingine, unasema hujawahi kuona je ni sheria ya mpira inakataza au ni haijatokea tu?kwa ufatiliaji wako wa soka umewahi sikia timu ina viporo 12
ama timu kucheza kila baada ya siku 2
ama backpass kuwa offside
ama mpira kuendelea ikiwa golikipa kaumia
Sio kazi ya TFF, Bodi ya Ligi au Marefarii kuzijengea uwezo baadhi ya timu kuchukua ubingwa. Uwezo unatokana na maandalizi ya kila timu moja moja, kuanzia usajili hadi training. Kumbuka mlivyokuwa mkibeza bajeti ya bilioni 1.3, mnadhani mambo yanajiendea kwa mazoea tu? Watu wamewekeza, viongozi wa timu hizo za Kagera Sugar na Lipuli pia wakitafuta fedha za kutosha maandalizi kama ya Simba, watatoa ushindani hadi wa kubeba ubingwa, na wala sio ajabu. Mbona Azam amebeba ndoo, tena zote ya Bara na ya Kagame Cup? Kwa kuwa aliwekeza katika usajili na uendeshaji. Yanga ilikuwa inagoma kufanya uchaguzi, sasa nani atawapa malezi wachezaji, kocha? Yaani kocha ameajiriwa uje umtegemee ndio awabembeleze wachezaji wasigome? Yanga mkubali kuwa hamkuwa na kikosi kizuri kama Simba, na hamkuwa na viongozi wazuri kama Simbamaandalizi ni kitu kimoja na ubingwa ni kitu kingine...chukulia mfano wa leister city ilivyotwaa ndoo ya uingereza...tunataka
kuwe na fairness teams kama Kagera shuga au lipuli ziwe na uwezo wa kuwa bingwa