Yanga ni ile ile haijabadilika jambo

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Anaandika @exaud_msaka_habari

Kwa mchezo wa Leo bado Yanga iliyomaliza wakati ligi inasimama na hii ya leo zipo sawa.

Ni kweli hatuwezi kuona matokeo ya Kocha Mwambusi kwa haraka ila bado ni ile ile.

Yanga inayocheza Soka la Kukimbizana sana kuliko Mipango, Kitu ambacho kiliwafanya KMC kuwa Huru sana kupiga Pasi nyingi

Yanga ya wachezaji wale wale wanaopoteza Mipira eneo ambalo unajiulIza kapotezaje

Yanga ambayo Wakijipanga waanze mpira nyuma anatokea mmoja wao anapiga mbele wanakimbizana tena

Yanga Yenye washambuliaji ambao bado wanakosa Magoli ya wazi sana

Yanga Ambayo Hata kocha alikuwa hajui anatafuta nini kwa wakati gani, Kumtoa Mukoko na Kumleta Nchimbi sijui hata kama na yeye alijua madhara yake pale katikati kwenda mbele

Hawajacheza Vibaya Ila hawajafanya vizuri sana hasa eneo la Mbele, kuna nafasi hatakiwi mtu anayecheza Yanga Kuzikosa

Tukisema tuwape muda ni sawa ila Ligi inasonga na hapo anatakiwa aje kocha Mpya afumue aanze na Mifumo yake

Yanga wanaangusha Point Mbili tena Nyumbani, sio ishara nzuri sana Kwenye lengo lao la Ubingwa

ALL IN ALL KILICHOBADILIKA MPAKA SASA NI RANGI YA NYWELE ZA FISTON
 
Tunaonewa ,tunahujumiwa, Simba inapendelewa....🤣🤣🤣🙌
 
Mnaeza makaendelea na mambo mengine mkatuachia yanga yetu sio lazima kila mtu aiseme
 
Kidimbwi kimetibuliwa tena kudadadeq
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…