Yanga SC bado tunamuhitaji Jerry Muro

kitumbotala

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
516
Reaction score
623
Wakuu habari zenu,

Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu,

Mimi kwa mtazamo wangu tunamuhitaji bado Jerry Muro awe msemaji wetu la sivyo tutaendelea kunyanyaswa kwa kauli za wakina Haji Manara.

Mpaka sasa sizani kama tuna msemaji wa Timu, maana kila siku kimya tuu yaani haiwezekani. Mechi ya juzi na watani wetu Simba tulitawaliwa vikali kuanzia kwenye mitandao mpaka majukwaani.

Mashabiki pia tunahitaji msemaji atakae amsha morali yetu sisi mashabiki.

Ni hayo tu kwa wana YANGA.

Karibuni ili tupaze sauti zetu.

***YANGA SC DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.***

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani unamlilia Jerry Muro ambaye alishindwa ku-update website ya klabu ?
 
Msemaji wa sasa yupo kisayansi zaidi. Nadhani matopeni ndiyo wanapaswa kuiga kwetu. Hizo ngonjera za Haji Manara sio saizi yetu mabingwa wa kihistoria Tanzania.
Lazima tuonyeshe tofauti yetu na wao. Umeziona post za Msemaji wetu kwenye FB. Brief, up to the point and informative.
 
Yeye hawaitaji nyie mnamuitaji acheni ujinga nyie watu wa Yanga..
 
Bahati mbaya propaganda nyingi za timu hizi huvuma sana katika redio na TV stations, na si katika mitandao. Hata Masau Bwire anapatia umaarufu katika Radio & TV Stations
 
Mkuu naheshimu hitaji lako. Ila Jangwani sio Bendi ya Taarab hadi tulazimishe huyo Khadija Koppa aje huku.

Umeona mambo ya Dismass Ten mitandaoni lakini...?
Mkuu Jumatano ulikuja na mbwembwe nyingi baadae ukapotea.....NDALA NI SHIDA...kazi ni kuendea MALIWATONI...
 
Dismas ni level ya kimataifa kwa kweli. Yanga imepata jembe kwa aina ya mashabiki wa Yanga walivyo, najua hatadumu muda mrefu kwenye hiyo nafasi. Usijekushangaa timu ikavurunda akasingiziwa yeye utadhani yeye ndio koch na mkuu wa benchi la ufundi
 
Mkuu Jumatano ulikuja na mbwembwe nyingi baadae ukapotea.....NDALA NI SHIDA...kazi ni kuendea MALIWATONI...

Sijawahi kupotea Jukwaani. Ukiona hivyo ujue niko na Majukumu ya Kifamilia. waulize wenzako hapa.
 
We una chuki zako binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sina chuki na Jerry.

Simjui na wala hanijui. So siwezi mchukia mtu ambaye sina uhusiano nao wa lolote. Ninasema kuwa muda wa mipasho na misemo ya kwenye khanga hakuna sasa hivi.

Huwezi kumuondoa Dismass ukamrudisha Jerry (kama unaujua vyema uwezo wa Dismass)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…