Yanga SC imetufundisha Simba mahesabu Kila hatua kimataifa

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
YANGA SC IMETUFUNDISHA MAHESABU KILA HATUA KIMATAIFA.

Klabu ya Yanga wametengeneza mahesabu makubwa sana kwenye mashindano ya Kombe la Mabingwa Afrika kwa kumaliza kinara wa kundi lake akiwa na alama 13.

Jambo hilo ni historia kwao na kwa Taifa kwa ujumla licha ya kwamba Simba aliwahi kuongoza Kundi Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya Al Ahly.

Kwenye mahesabu wamepata faida mbili kubwa, Yanga wamepata faida ya kwanza ni kutokutana na waliomaliza nafasi ya kwanza katika makundi ikiwa watamaliza hivyo.

Faida ya pili ni kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani mchezo wa robo fainali. Sio kila klabu imeweza msimu huu.

Yanga imechukua alama 6 muhimu kwa TP Mazembe na kuwa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kupata ushindi kwenye dimba la TP Mazembe. Yanga wameonesha kuwa wao ni bora sana popote wana shinda.

Yanga inatengeneza bond kubwa na CAF kwa kasi mno. Jitihada za GSM, wanachama mpaka mashabiki wameamua kuwa pamoja kutafuta mafanikio zaidi kimataifa, wachezaji wanajituma sana dimbani.

TP Mazembe walifanya kila kitu lakini Young Africans walifanya kila kitu kwa usahihi! approach nzuri imewapa matokeo. Yanga wamefanya vizuri sana kwenye hatua ya Makundi, hii ni kutokana na ubora wa kikosi chao.

NB: Maendeleo hayana Chama ...sisi wanasimba tujifunze kitu

 
Kwahiyo yote aliyofanya Yanga mwaka huu simba hajawahi kufanya au kuwa na hizo rekodi.

Km simba alishafanya Nani wa kumfundisha mwenzake?

Na ni nani kakwambia Yanga anacheza klabu bingwa?

Hakuna utopolo mwenye akili!
 
Utopolo rudia ulichoandika, halafu rudi uniambie km pale utopoloni Kama wenye akili wameongezeka toka wale wawili watangazwe.

Duuuuh!
 

Ndio umenunua cm ya smartphone
 
Kumbe yanga Wapo kombe la Mabingwa Africa
 
Kwahiyo yote aliyofanya Yanga mwaka huu simba hajawahi kufanya au kuwa na hizo rekodi.

Km simba alishafanya Nani wa kumfundisha mwenzake?

Na ni nani kakwambia Yanga anacheza klabu bingwa?

Hakuna utopolo mwenye akili!
Alifanya Kwa kutumia ndumba sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…