Yanga SC rudisha Mrisho Ngasa tafadhali

Yanga SC rudisha Mrisho Ngasa tafadhali

yahoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
3,526
Reaction score
1,409
Tangu nilivyoifahamu Yanga enzi za sanifu Lazaro, akaja Lunyamila, wakafata wengine na wengine hadi juzi kati Msuva. Tulikuwa tunashambulia kwa kasi kupitia pembeni miaka nenda rudi, huo ndo utamaduni wa timu yetu.

Lakini timu yetu ya mwaka huu inatofauti na Yanga zote zilizopita ndo mana tunapata ushindi wa magoli machache. Tunapata goli kwa tabu sana, hii ni kwa sababu tunashindwa kushambulia kwa kasi kupitia pembeni. Ni lazima tupate wachezaji wenye kasi kupitia pembeni, huyo mchezaji tukishindwa kumtengeneza tumrudishe Mrisho Ngasa kwanza wakati tunajiuliza.

Ngasa bado mchezaji mzuri tu kibongobongo, tusidanganyike eti kwasababu amefeli huko south Africa ndo hatufai, mbona kunamchezaji mmoja wa Simba anafanya vizuri tu ingawa huko alikotoka hakupewa nafasi hata ya kukaa bechi. Halafu Ngasa anaijua Yanga vizuri na anacheza kwa moyo..

Wako kwenye ujenzi Wa Dar young Africa..
 
Kilio changu kwa yule kocha......wamtimue kwa kweli ni kimeo ...msimu huu naona tunashika nafasi ya tatu
 
Yanga ya mwaka huu sio kabisa! Yaani wafanye mapema sana kuwanoa na kuwapanga vizuri wale wachezaji kwenye kushambulia na umaliziaji.

Kama vipi wamrudishe pia Hans Van der Pluijm.
 
  • Thanks
Reactions: p84
Tatizo sio kocha. Muda mrefu sana formation ya timu ilikuwa around Simon Msuva kama Ngasa enzi zake. Lazima tukubali mabadiliko
 
Kila mchezaji duniani, kuna sehemu yake akicheza huwa na nyota...Mrisho Ngassa hata aende wapi akicheza Yanga atacheza vizuri. Kwahiyo ni wazo zuri, na saivi tukimchukua huyu hana gharama kubwa, sababu ni mpenzi wa yanga, na aliko kule ni kwasababu ya maisha tu. Ila wampe hata mwaka mmoja atatoa mchango mkubwa kuliko kuwa na makinda ambao hata hawapewi namba.
 
Yanga wenyewe wanasema eti miaka yote huwa wanaanza mdogo mdogo nafasi ya kumi na moja. Waache waendelee wakidhani wataamka baadaye, nakwambia watashuka daraja
 
Yanga wenyewe wanasema eti miaka yote huwa wanaanza mdogo mdogo nafasi ya kumi na moja. Waache waendelee wakidhani wataamka baadaye, nakwambia watashuka daraja
Hujui mpira wewe,,,,nenda kacheze usolo kijijini kwenu.
 
Kila mchezaji duniani, kuna sehemu yake akicheza huwa na nyota...Mrisho Ngassa hata aende wapi akicheza Yanga atacheza vizuri. Kwahiyo ni wazo zuri, na saivi tukimchukua huyu hana gharama kubwa, sababu ni mpenzi wa yanga, na aliko kule ni kwasababu ya maisha tu. Ila wampe hata mwaka mmoja atatoa mchango mkubwa kuliko kuwa na makinda ambao hata hawapewi namba.
Angalau wakishindwa kumrudisha ngasa basi wamtengeneze Matteo Anton nahisi anaweza kuwa na Kariba ya msuva na ngasa lakini cha kushangaza hawampi namba
 
Hujui mpira wewe,,,,nenda kacheze usolo kijijini kwenu.
Kuujua kwa maana ya kuucheza? Mbona mapovu? Kumbuka, kuna makocha na viongozi wa vyama vya soka duniani ambao hawajawahi kuucheza mpira wa ushindani kiwanjani, lakini ni mameneja wazuri kabisa. Kama thread hii ingekuwa ni kwa ajili ya wachezaji tu, ningeondoka, lakini nipo na nasubiri huo mdogo mdogo utakapokuwa mkubwa mkubwa
 
Tatizo si kocha ni skilled players kulingana no zao
 
Meneja wa Yanga nae inabidi ajitathimini...ni wa mda mrefu pale clubuni...sijui kama bado anafit.
 
Back
Top Bottom