Yanga SC tunaibiwa mchana kweupe

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Ni nani hasa anayeruhusu uhujumu uchumu wa Klabu ya Yanga SC kwenye suala zima la jezi.?

Ni kiongozi yupi wa Yanga SC asiyejua kuwa suala la jezi lina maslahi mapana kwa klabu.?

Nimekuwa nikifuatilia hizi jezi Mpya za Yanga ambazo zinasemekama zinaenda kutumia msimu ujao wa 2017/18. Hizi jezi zinauzwa kama njugu, cha ajabu zaidi ni kwamba Klabu haipati mgawo wowote ule kutoka na na mauzo ya Jezi hizi.

Ni tofauti sana wanavyofanya klabu kubwa nyinginezo ambapo percentage ya mauzo ya jezi ya klabu husika yanarudi klabuni. Hivyo kuifanya klabu kuwa na chanzo cha ziada cha mapato.

Ebu Fikiria: Jezi moja tu inauzwa kwa Tsh 20,000/= ambapo hakuna hata senti 5 inayoingia klabuni. Ni biashara gani hii wanayoifanya YANGA SC?



Bila shaka kuna kiongozi mule ndani anahusika moja kwa moja na dili hili ambapo kwa story za chini ya kapeti zinasema yeye pekee anavuta ka'mkwanja kwa kuidhinisha utengenezaji wa hizi jezi na huyo mzalishaji.

Nataka viongozi wangu watambue kuwa Yanga ni Brand kubwa sana, iweje suala la jezi linamnufaisha mtu binafsi na sio klabu. Na hapo hapo tunalazimika wanachama kuchangia klabu inapoonekana hakuna pesa za kutosha kuendesha klabu.
 
Kila Mbuzi ale kwenye urefu wa kamba yake.
 

Umeongea kwa uchungu sana kiongozi.
Na ndio maana watu awataki mabadiliko
 
Komaa na miradi yako. Mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenyewe.
 
Umeongea kwa uchungu sana kiongozi.
Na ndio maana watu awataki mabadiliko
Hili suala si lazima liambatane na MABADILIKO...

Kuna mpuuzi pale anapiga pesa tu.
 
itabidi Yanga labda mfanye ule u-Msama. unamkumbuka Msama na kazi za wasanii??
 
Mfumo wa uendeshaji wa mpira nchi hii ni wa ajabu sana. Timu hizi zinalalamika ukata wakati biashara iliyo wazi kama hii inafanywa bila kunufaisha klabu. Mashabiki na wanazi wa hizi timu wabadilike na kuleta shinikizo kubwa kwa viongozi ambao inaonekana wana maslahi na magumashi yanayoendelea.

Simba walijaribu na kuonyesha mwanga kidogo lkn sasa hivi haijulikani wameishia wapi. Kwenye mikutano sijui kama taarifa za mapato zinaonyesha mauzo ya jezi yameleta sh ngapi na kuna mkakati gani wa kuboresha
 
Huu utaratibu mbona upo miaka yote,ulikuwa unaishi ughaibuni nini ?
 
Huu utaratibu mbona upo miaka yote,ulikuwa unaishi ughaibuni nini ?
Sikuwahi ona Uhlsports wakifanya mauzo ya jezi za Wateja wao....

Labda utaratibu upi unao uzungumzia wewe.
 
Yaani Haya maviongozi ni ziro kabisa.
 
Soka la TANZANIA lita piga hatua mpaka mzungu aje atutawale kwa awamu ya 3
 
Sikuwahi ona Uhlsports wakifanya mauzo ya jezi za Wateja wao....

Labda utaratibu upi unao uzungumzia wewe.
UhlSports ndio wanatengeneza hizo jezi zilizopo Kariakoo ?

Ukienda Uwanja wa Taifa mbona hizo jezi zinauzwa miaka yote
 
Hivi ni tangia wana Yanga walikuwa na ' akili ' za Kimaendeleo?
Mla pupa hadiriki kula tamu. Sahihisha sentensi yako kwanza ili ilete maana kabla haijabainika kwamba hilo unalowakusudia Wanayanga kwako limezidi maradufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…