Yanga & Simba kwa makocha hawa asilimia 50 heshima ya nchi kwenye soka itashuka

Yanga & Simba kwa makocha hawa asilimia 50 heshima ya nchi kwenye soka itashuka

witacha matiku

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
722
Reaction score
237
Umofia wana Jukwaa.
Binafsi nasikitika na trend ya timu zetu kimataifa hadi sasa hamna unafuu kwa Timu zetu Kati ya Simba na Yanga.

Kuna shida hasa kwenye management Simba iliwaza nini kumsajili Kocha ambae haja- prove kokote alikuwa Kocha namba 2 Raja na hakuna cha maana alionyesha kwa mafanikio ya timu vilevile Yanga Kocha hajashinda game sita (6) consecutively ni Sare na vipigo unamleta a- train Timu icheze na National Al ahly kweli ?

Triple C alionyesha uwezo wake umepungua pia kiberenge/ chapombe kutoka Ghana alishindwa akiwa Simba plus Mkude nishati imepungua lakini Hersi kisiasa za ushabiki akatoa pesa nyingi akawapeleka Jangwani hadi Leo kuna madeni, kulikuwa na umuhimu gani wa kusajili rejected players ?

Timu ipo kwenye mashindano unamfukuza Kocha mwenye experience unaleta Sangara as if Avic Town ni mto wa kufuga samaki.

Game ya Leo 08.12.2024 ilikuwa Simba ishinde na hapa ndio ukubwa wa Timu unakuja lakini Kocha anaingia na mentality ya kulinda na kusababisha kuanza kutegeana kwa mabeki na kujikaba wenyewe though Simba imeonyesha game nzuri lakini Kocha au uongozi wa Simba utoe ushauri kwenye bench la ufundi Ahoua anachoweza ni kuzunguka na Pacome kwenye clubs sio kucheza, Dogo pimbi sana hana anachofanya uwanjani, mchezaji bamia sana zero brain hajui anafanya nini uwanjani.

Ahoua kwa namba anayocheza hana msaada kwa timu. Ni mchezaji liable / weak sana number TEN inatakiwa uwe jitu la mavitu na utulivu wa kutosha.

Kocha ana changamoto ya kupanga kikosi na hiyo ni kwa sababu ya kuamini kulinda zaidi na kupelekea wachezaji kukosa umakini langoni mwa mpinzani.

Ahoua kwa sasa ni mzigo kwa Timu kitendo cha kocha kumweka nje AWESU ni kutukosea mashabiki huyu mchezaji wake hana sifa ya kucheza hata Tabora United. Mchezaji hana hatari langoni mwa mpinzani utulivu zero , Passing zero & dribbling zero so what kind of professional player is this ?


Kocha anatukosea sana Simba fans AWESU yupo Deborah ana utulivu mzuri anaanzia benchi kweli ? Ahoua must Go anawakaba wenzake.

Kama tutaendelea hivi soka letu litarudi nyuma sana kwa sababu nina hakika Yanga hatoboi makundi kwa nature ya wachezaji waliopo na Kocha wao. TX Galax kwa sasa inafanya vizuri lakini kipindi cha mbegu ya maboga Timu ilikuwa tangawizi kumbe shida ilikuwa ni Kocha.

Nawaza possibly tumeshaushiwa na wahuni ili tulete hawa makocha ili thamani ya league yetu ishuke "conspiracy"
 
Timu zetu bado hazina wadhamini wanaoweza kuingia sokoni na kuvuta vyuma vya maana ikiwemo makocha, na mashabiki ndo kabisa kelele nyingi ila mchango mdogo.
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Mipang'ang'a SC.
4. Malalamiko (Lialia) SC.
5. Makelele SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyaunyau (mapaka) SC.
8. Mwakarobo SC.
9. Mikia SC.
10. Miso Misonda SC.
11. Manyang'au SC.
12. Mazumbukuku SC.
13. Mazombi SC.
14. Kinyume nyume SC.
15. Ngada SC.
16. Kolowizard SC.
17. Zuwena SC.
18. Bebwabebwa (Mbeleko) SC.
19. Panya roads SC.
20. Kikanuni SC.
21. Kufa Kiume SC.
22. Ubaya ubwege SC.
23. 5imba SC.
24. Visingizio (Visababu) SC.
25. Manguruwe SC.
JamiiForums-312072181.jpeg
 
Kiufupi Yanga hakuna kocha na Simba hakuna Kocha. Club zetu mwaka huu zinashuka viwango zote. Simba Kocha mbovu, wachezaji tumepigwa(Mutale, Ahoua, Karabak, hakuna kitu), Yanga usajili wao pia mbovu, na Kocha mbovu.
 
Mbona mnawapanikisha watu mnamlaumu kocha wakati wachezaji kawakuta, usajili wamefanya viongozi still bado mnawalaumu makocha.
 
Tatizo la kocha wa simba ni upangaji mbovu wa kikosi na kumwamini mchezaji asiye na uwezo jean charles ahoua
 
Hakuna kocha pale, Ahoua kazi kushindana kunywa Konyagi kavu na kushinda kitambaa cheupe, Ateba anakimbia kimbia tu hajui hata formula za offside amebaki kuwa striker la penalty, Mutale hajui hata anachezea timu gani 😀 Karabou hapati namba Pamba jiji, Debora hajui anacheza namba 10 au anaosha vyombo jikoni
😀 NB; Mpaka sasa kwa timu inayojielewa ilipaswa kuwa imeshajipata vyema, ila hapa tumepigwa! Ni vile tu mpinzani naye anapitia kipindi kigumu
 
Kwani fadlu ndo kamsajili ahuwaa? Kama kibu hana uwezo wa kufunga na kuasisti unataka fadlu afanyaje? Hamza kajifunga mwenyewe kwa kushindwa kujiposition ulitaka fadlu afanyaje? Walaumu viongozi wako kwa kusajili magarasa.

Simba tulitaka kumsajili sergi pokou al hilal wakaongeza dau wakamchukua tukaenda kulisajili garasa mutale.

Simba tulitaka kumsajili kiungo namba 10 tishio afrika abdelhay forsy kutoka moroco zemamara wametaka milioni 800 tumekimbia.

Feitoto hadi sasa hivi tumeshindwa kumsajili.

Tunaishia kusajili magarasa tu.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Hakuna kocha pale, Ahoua kazi kushindana kunywa Konyagi kavu na kushinda kitambaa cheupe, Ateba anakimbia kimbia tu hajui hata formula za offside amebaki kuwa striker la penalty, Mutale hajui hata anachezea timu gani 😀 Karabou hapati namba Pamba jiji, Debora hajui anacheza namba 10 au anaosha vyombo jikoni
😀 NB; Mpaka sasa kwa timu inayojielewa ilipaswa kuwa imeshajipata vyema, ila hapa tumepigwa! Ni vile tu mpinzani naye anapitia kipindi kigumu
Mc alger 2 Yanga 0

Al hilal 2 Yanga 0

Tabora 3 Yanga 1

Azam 1 Yanga 0

Mechi 4 magoli ya kufungwa 8.
 
Timu zetu bado hazina wadhamini wanaoweza kuingia sokoni na kuvuta vyuma vya maana ikiwemo makocha, na mashabiki ndo kabisa kelele nyingi ila mchango mdogo.
Hivi unaamini kweli usajili wa Simba uligharimu bilioni Saba, usajili ni scout nzuri na sio kutumia pesa nyingi na kocha mzuri snachangua kiasi kubwa matokeo ya timu
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kama vipi Mangungu atuachie tu timu yetu. Mzee Kilomoni anatufaa zaidi.
 
Back
Top Bottom