Yanga Trust the Process

Yanga Trust the Process

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Yanga msivunjike mioyo, uaminini mradi mliyoanza kuujenga, inatakiwa mkubali bado ni changa inaendelea kukua.

Timu inacheza vizuri cha msingi ni kuboresha sehemu ndogondogo zilizosalia hasa ulinzi.

Wekeni nguvu kwenye Michuano ya Shirikisho huenda huko mkafika mbali.

Msikubali kukatishwa tamaa, endeleeni kujaribu tena na tena, keep pushing.

Waswahili wanasema "Jitihada hazimtupi mkulima".

Hakuna kipindi ambacho mashabiki wa Yanga mnapaswa kuwa karibu na timu kama kipindi hiki.

Mtatupiwa uchafu wa kila aina, mkikubali kwenda na upepo mtaivuruga timu ambayo imeanza kuonesha mwanga.

Kukata tamaa ni dhambi. Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi.

Muelewe giza linapozidi ujue pamekaribia kupambazuka.

Yanga, Trust the process. [emoji119]
 
Ila pia uwashauri wasiendelee kuwekeza kwenye kupiga domo, mpira ni sanaa na sio longolongo hasa huko kwenye michuano mikubwa, usiendelee kuwatia moyo bila kuwaambia ukweli.
 
Uto hawa amini macho yako ukizingatia yule mzungu pori aliwa aminisha wanaenda kufika mpaka fainali ya mabigwa baada ya kuwafunga wale wahuni wa zalani.
 
Ushauri mzuri, ila swali je wana plan za execute hio process yao? Nadhani mna bahati kuwa na Rais msomi na mwenye exposure nzuri, kazi ni kwake kugeuza hali hii.
 
Yanga msivunjike mioyo, uaminini mradi mliyoanza kuujenga, inatakiwa mkubali bado ni changa inaendelea kukua.

Timu inacheza vizuri cha msingi ni kuboresha sehemu ndogondogo zilizosalia hasa ulinzi.
Uchezaji mzuri uambatane na matokeo chanya. Ikiwa matokeo ni hasi, binafsi sioni mantiki ya kuwasifia kuwa timu inacheza vizuri.
Wekeni nguvu kwenye Michuano ya Shirikisho huenda huko mkafika mbali.
Ni mambo gani yafanyike ili timu ya Yanga ifike mbali? Unaposema "wekeni nguvu", unamaanisha nini?
Jaribu kuchambua mambo kwa upana wake, wacha kuzungumzia holistic approach.
Msikubali kukatishwa tamaa, endeleeni kujaribu tena na tena, keep pushing.

Waswahili wanasema "Jitihada hazimtupi mkulima".

Hakuna kipindi ambacho mashabiki wa Yanga mnapaswa kuwa karibu na timu kama kipindi hiki.

Mtatupiwa uchafu wa kila aina, mkikubali kwenda na upepo mtaivuruga timu ambayo imeanza kuonesha mwanga.

Kukata tamaa ni dhambi. Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi.

Muelewe giza linapozidi ujue pamekaribia kupambazuka.

Yanga, Trust the process. [emoji119]
 
Ungetoa ushauri huu kabla hawajatolewa nakuhakikishia wangekutukana matusi yote,ila kwakua wametupwa nje ya caf champions watakusikiliza.
huwa ni wabishi sana hawa jamaa.
 
Back
Top Bottom