Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,669
- 8,268
Yanga msivunjike mioyo, uaminini mradi mliyoanza kuujenga, inatakiwa mkubali bado ni changa inaendelea kukua.
Timu inacheza vizuri cha msingi ni kuboresha sehemu ndogondogo zilizosalia hasa ulinzi.
Wekeni nguvu kwenye Michuano ya Shirikisho huenda huko mkafika mbali.
Msikubali kukatishwa tamaa, endeleeni kujaribu tena na tena, keep pushing.
Waswahili wanasema "Jitihada hazimtupi mkulima".
Hakuna kipindi ambacho mashabiki wa Yanga mnapaswa kuwa karibu na timu kama kipindi hiki.
Mtatupiwa uchafu wa kila aina, mkikubali kwenda na upepo mtaivuruga timu ambayo imeanza kuonesha mwanga.
Kukata tamaa ni dhambi. Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi.
Muelewe giza linapozidi ujue pamekaribia kupambazuka.
Yanga, Trust the process. [emoji119]