Yanga tumekuwa wakiwa sana tangu Hans aondoke Yanga na Lwandamina kukabidhiwa mikoba.

nadhani wameshiba mafanikio mkuu.
ubingwa mfululizo miaka mitatu uwewachosha nadhani, labda kama wangesajili kikosi kipya 60%.
si unawaona Real Madrid kwenye La Liga nao wanavyosuasua baada ya mafanikio ya mfululizo?
 
Yanga ya Hans wachezaji walikuwa wanalipwa mishahara kwa wakati.
Yanga ya Lwandamina mishahara ya kusuasua
Yanga ya Hans wachezaji awajawai kugoma kwa ajili ya malipo
Yanga ya Lwandamina wachezaji wa shagoma kufanya mazoezi sababu ya kucheleweshewa malipo
Msimu uliopita chini ya Hans timu ilikuwa ipo chini sana katika uchezaji hadi ikifikia watu kuanza kuhoji uwezo wake.

Lazima tukubali wapenzi wa Yanga hiki ni kipindi cha mpito tuvumilie. Na tujifunze kupitia kwa wenzetu pindi akitokea mtu au watu kutaka kuibadili club kuelekea katika kujitegemea tusiwe tena na maneno kuwa hii ni Yanga yetu tumetoka nayo mbali atutaki kumpa mtu aua watu, wakati atuwezi kuisaidia club wakati wa matatizo.
 
Huu ni mwaka wa shida. Ninavyoona lile gundu la Simba limehamia kwetu.

Mkuu sembo ni mtaalam wa kuwa eneo korofi, naomba utufundishe namna ya kulifikia hilo eneo korofi maana mwaka huu tutalitafuta sana.
 
Tamaa ya kumfunga mwarabu ndiyo iliyofanya Hans afukuzwe Yanga,walikuwa wanadai kuwa Lwandamina ana uwezo mkubwa sana wa kuwafunga waarabu.
inasikitisha sana

Sent From My iDevice using Jamii Forums Auto-reply Mobile App
 
Namlaani aliyetoa wazo la kumuondoa Babu na kutuletea huu mwili mkubwa kama sausage ya kuchoma. Hamna chochote anachofundisha, huu ndio mwanzo wa mikia kulia mbwata
 
Haya sasa huyu aliyeletwa kwa mbwembwe ndio atatukosesha hata hiyo tiketi ya kushiriki...hovyo kabisa hilo dude
 
Sema toka Manji aondoke sio Hans. Sasa hivi kuna njaa!
 
Kule Mabingwa hakuna kuhonga.
 
Tulijua utakuwa mchezo mgumu, kipindi cha pili tulilazimika kubadili mbinu ili kukabiliana na mazingira, Nawashukuru wachezaji hakika walifanya kazi kubwa dakika zote 90...GL
 
Pamoja na uwasilishaji mbovu wa mleta thread, hii haiondoi ukweli kuwa Yanga hali yetu ni mbaya tangu Hans Van Plujium kuondoka.
 
Tuwe na subira muda ni mwalimu mzuri Sana Kama ni mbovu itajulikana tu huwez kumwita mtu mbovu wakat amekupa ubingwa... Tusubir Baada ya mechi walau tano tuone itakavyokuwa.. Mana amejnasibu kuwa msimu huu ndo anatumia mbinu zake Tusubiri Kidogo jaman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utadhani mkipewa timu mtaweza lolote......ovyoooo
Kuweni wavumilivu!
Inawezekana wachezaji ndo hawajitumi!
Msisahau kuwa hata wachezaji wana mioyo ya nyama, kilichotokea kwa Manji naamini hata wachezaji kimewaathiri kisaikolojia, tunatakiwa kuwatia moyo wachezaji na si kuwaita wanadamu wenzetu "bundi"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hongereni sana.mmempata
 
Mimi nawashangaa wanaosema Yanga haiko vizuri kiuchumi,ilikuwaje wakaongeza wachezaji wapya wa kimataifa kama hali si nzuri na wao wanalijua hilo.Huyo kocha mwenyewe kaongezewa mkataba mwingine wakati wakijua kabisa wana hali mbaya.Kama ndiyo hivyo wangeachana na hizo gharama za kocha na wachezaji wapya wa kimataifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie siwezi kumsema sana Lwandamagere ila nachoweza kuisemea timu yangu Yanga ni kwamba Hans alitufaa sana. Alitusaidia sana na tokea kaondoka pengo lake ni kubwa kuliko hata la kuondokewa na wachezaji kama akina Msuva. Tulipoteza kocha baada ya kuwa tumelewa sifa za vikombe na sasa sijui kama tutaambulia hata ka kikombe kokote mwaka huu. Tulipoteza kocha. Siku zote binafsi nitamkumbuka sana Hans
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…