Yanga tununue magoli uwanjani

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mashabiki watazamanaji wa mechi za Yanga viwanjani tuanzishe utamaduni wa kuchangia hapo Kwa papo uwanjani kadri mtu anavyoweza kupata pesa za kununua kila bao linalofungwa na mchezaji na kila aliyetoa pass ya goli.

Nawasilisha.
 
Mashabiki watazamanaji za Yanga viwanjani tuanzishe utamani wa kuchangia hapo Kwa papo uwanjani kadri mtu anavyoweza kupata pesa za kununua kila bao linalofungwa na mchezaji na aliyetoa pass ya goli.

Nawasilisha.
Anza were mkuu tukunge mkono, ni wazo zuri, na hii isiwe kwa mechi ya Tar 30 tu, kila mechi mpango huu huuusike, naunga mkono hoja 100% mkuu.
 
Anza were mkuu tukunge mkono, ni wazo zuri, na hii isiwe kwa mechi ya Tar 30 tu, kila mechi mpango huu huuusike, naunga mkono hoja 100% mkuu.
safi mkuu, matawi ya yanga yaratibu mpango huu wa papo kwa papo wa mashabiki wa yanga na kuufikisha kwenye uongozi wa yanga ili nao pia wafahamu na kushirki katika utamaduni huu mpya wa kuwatia hamasa wachezaji wetu. Kushangilia tyuuuu sawa lakini nadhani hakutoshi kumtia utambi mchezaji anaekupatia raha ya goli. Itadhihirisha kwa vitendo kuwa Yanga ni timu ya wananchi wote. Tukizoea utamaduni huu wa kuichangia starehe yetu ya mpira hata wadhamini hawatatuyumbisha sana kupita kiasi. Mpira ni ghali.
 
Tangu nianze kuichangia Yanga kupitia simu yangu ya mkononi ninajisikia kuwa na mimi ni sehemu ya mafanikio ya Yanga, furaha yangu imeongezeka mara dufu kuliko zamani. Jaribu uone utakubaliana na mimi kwenye hili. Yaani kuwa mshabiki tyuuuuu na kuwa mshabiki aliyechangia japo 1000. Lazima utajisikia u-ownership fulani wa mafanikio ya club na hasa pale unapomuona mchezaji anayevuja jasho jingi uwanjani anatafuta japo funda 2 tu za maji ya kunywa akate kiu ili aendelee kukupa burudani uwanjani. Naona kama ile 500 yangu niliyochangia ndiyo iliyonunulia yale maji aliyopewa mchezaji uwanjani pale.
 
Mashabiki watazamanaji wa mechi za Yanga viwanjani tuanzishe utamaduni wa kuchangia hapo Kwa papo uwanjani kadri mtu anavyoweza kupata pesa za kununua kila bao linalofungwa na mchezaji na kila aliyetoa pass ya goli.

Nawasilisha.
wazo zuri nani akusanye?
 
wazo zuri nani akusanye?
wazo zuri nani akusanye?
Changamoto ipo hapo, maana tunataka pesa zote ziwafikie walengwa hapohapo uwanjani baada ya mechi na siku hiyohiyo bila ya kuingia kwenye mifuko ya watu wengine. Hebu toa ushauri wako hapo unadhani nini kifanyike kwenye kufanikisha hili? Lakini nadhani sio ngumu, kama watu wanaweza kuwatuza waimbaji wa taarab jukwaani ukumbini kwnini sisi tushindwe wakati wafungaji na walioassist tumewaona kwa macho yetu? tena kama tungefahamu simu zao hata watazaji kwenye luninga na wasikilizaji kwenye redio wangewajaza pesa hukohuko vibanda umiza waliko
 
Mkuu mabeki je na kipa ambao watajituma ila watashindwa kufunga au kutoa assist kulingana na nafasi zao mnawasaidiaje kwenye huo mgao.?
 
Mkuu mabeki je na kipa ambao watajituma ila watashindwa kufunga au kutoa assist kulingana na nafasi zao mnawasaidiaje kwenye huo mgao.?
ndiyo, lakini mpira ni magoli, duniani kote wanaheshimu magoli ingawa timu yote imecheza uwanjani. Ona mchezaji mmoja anvyoruhusiwa kuondoka na mpira peke yake baada ya kufunga magoli 3 kwenye mechi. Je, mbona huulizi kuhusu wale waliompa pass na wachezaji wengine wenzake aliovuja jasho nao. Hiyo ya kuwa wachezaji wote ni ngumu hata FIFA wameshindwa kuitekeleza. Ndiyo maana kuna mtu anayeitwa man of the mechi ambaye ni mtu mmoja tu.
 
Bora huyo man of the match ndie mngempa zawadi kwani anaweza kuwa kipa,beki, kiungo au forward
 
Bora huyo man of the match ndie mngempa zawadi kwani anaweza kuwa kipa,beki, kiungo au forward
Utajuaje hasa kama huyu ndiye aliyestahili kuwa man of the match? Kila mtu anakuwa na mtu wake ndio maana kuna majadiliano ya kumtafuta man of the match. Lakini mfungaji hana ubishi kila mtu anamjuwa hapohapo. Wacha wadau wengine wahangaike pia na motisha wa wachezaji wengine wote, sisi mashabiki watazamaji let us focus kwenye striking department for more goals. Hata mechi yetu na Stand United kilichotunusuri ni idadi kubwa ya magoli tuliyofunga tukashinda 4-3, vinginevyo tungeadhibiwa na wale watoto.
 
We ndo mzee akili mali nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…