Yanga Uamuzi Wa Kukurupuka, Mngeomba Maoni Kwanza

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Inawezekana kabisa hao walioamua kuondoa benchi lote la ufundi ndio hasa waliostahili kuondoka!

Benchi hilo mnaloliondoa nani aliliweka?vipi kuhusu gharama?

Naona kama Yanga ilikua hatua tisini mbele sasa itarudi nyuma hadi hatua arobaini.

Hivi mfano hata mtu una basi lako ila linasumbua kwenye kupiga starter lakini linasafiri vizuri safari ndefu za mikoani kutatua shida hiyo utauza gari?au utatafuta sababu kama ni battery au altorneter au wiring?

Uongozi wa Yanga mngetulia kutafuta sababu au Mngeomba ushauri kwa wadau na washabiki nini kifanyike. Timu imepoteza mchezo mmoja tu hadi sasa na timu inaongoza ligi shida iko wapi? Kaze kosa lake kuongoza ligi? Wachezaji wa Yanga hasa wazawa na mtu kama Niyonzima bado wana hadhi ya kuichezea Yanga ya kiwango mkitakacho?

Hebu tafuteni fungu muongeze wachezaji ma pro toka Ghana,Mali hata Morocco kama kweli mnataka matokeo.

Kwa kweli mmekurupuka viongozi wetu na sasa ndio mmeshatengeneza shida zaidi klabuni.
 

Hao Mashabiki unaotaka waombwe ushauri si ndiyo hawa walioanza kumkataa Kocha na kushinikiza atimuliwe? Au unazungumzia Yanga ipi Boss?

Your browser is not able to display this video.
 
Ngoja tuone kwanza kitakacho tokea baada ya hilo benchi la ufundi kuwekwa kando. Mchawi halisi atajulikana tu. Kama ni hilo benchi la ufundi, wachezaji wazembe, viongozi au wadhamini!!

Kimsingi tungependa kuona timu yetu ikicheza vizuri na pia kupata ushindi ili ikiwezekana tuchukue ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
 
Kumtetea Kaze kunahtaji nguvu ya kujitoa mhanga. Kocha asiye na first eleven ulimwona wapi ulimwengu wa sasa?
 
Mjomba ni heri ufungwe mechi moka ushimde nne au tano mfulizo kuliko mwenzio anafungwa 2 anapoteza point 6 anashinda zote zinazofatia wewe unatoa sare mechi 4 umashinda moja unafungwa moja piga hesabu nani kapoteza point nyingi..

Kumbuka sare pia ni kupoteza point 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…