Yanga vs Simba tarehe 8 March, 2020

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
780
Wapenda mpira siku ya jumapili wiki hii kutakuwa na mtange wa kukata na shoka kati ya Yanga na Simba tar 8 march 2020. Kama kawaida kila upande huaamini timu yao bora.

Naanza na uchambuz huu kuidadavua hii mechi.

Nitaanza na Yanga, kwa takribani wiki mbili sasa yanga wamekuwa kwenye ubora mzuri wa kupata magoli ktk mechi zao zilizopita kutokanana na baadhi ya wachezaj waliosajiliwa Jan kuanza kuzoeana na wenzao.

Ubora wa Yanga: Timu ya yanga inaonekana kuwa bora pembeni mwa uwanja kupitia kwa morrison na mipira mingi sana wanaipitishia huko lakini pia kupitia kwa haruna. Timu imekuwa ikipata magoli kupitia huko kwa kumshirikisha sana tshishimbi.

Uzoefu wa yanga: Yanga tatizo kubwa ni beki zake kufanya makosa mara kwa mara pale ambapo timu pinzani ikishambulia kwa cross nyingi hii imeonyesha namna gani hawajaweza kufanyia kazi.

Kipa: Wana kipa bora sana kwa sasa tatizo lake ni mipira ya kona.


Kwa analysis hii kama yanga wataweza kutulia upande wa beki zao wananafasi nzuri ya kupata draw au ushindi


SIMBA: Simba imekuwa bora tangu watoke kwenye mashindano ya mapinduzi cup baada ya kupata lawama nyingi sana kutoka kwa mashabiki wao mpaka ikafikia hatua MO kujitoa lakini baadae akarejea.

UBORA WA SIMBA: Ubora wa simba upo kwa mwamba wa lusaka na mkenya kahata wamekuwa na pass za hatari sana bila kumsahau mtawanya mipira mkude...Simba wamekuwa wakipitisha mipira yao mingi sana kwa Chama ili kufanya mashambulizi. Uwepo wa chama kahata na mkude ktkt inawapa simba jeuri ya kuicontrol game.

Udhaifu wa simba: Simba wanatatizo la beki kama ndugu zao yanga hasa pale kocha anapokosea kuwapanga vzr...naamini morisson atawasumbua sana mohamed hussein kwa sbb tshabalala anapenda kupandisha mashambulizi hii ni hatari kwa mipira ya haraka haraka ya yanga.

Kipa: Kipa wa simba amekuwa imara sana tangu awekwe benchi kwa mechi kadhaa japo anatatizo la kudaka mipira ya mbali kwa hiyo Yanga wanaweza kutumia huu udhaifu kupata magoli. Manula amekuwa bora sana mipira ya kona cross zote na tich for touch.


Mwisho
Timu itakayofanya makosa itaadhibiwa kwani kila timu imekuwa imara kipindi hiki kuanzia mwishoni mwa Jan.

Simba nawapa 60% ya kushinda
Yanga nawapa asilimia 40%
Draw ni asilimia 80%

Karibuni tudadavue kabla ya mtanange wenyewe.

Mchambuzi wa soka la bongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mikia fc a.k a mihamala fc wanakufa
 
Umejitahidi kuficha hisia zako ingawa hukwenda sana deep .Nakubaliana na percentages ulizotoa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Morrison hachezi upande wa Tshabalala, atakumbana na Kapombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…