Yanga walizoea vya kunyonga, sasa kila mechi lazima walalamikie waamuzi tu

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Kipindi cha Malinzi ilikuwa aibu kubwa sana kwa nchi kwa jinsi waamuzi walivyokuwa wakichezesha.

Msimu uliopita na msimu huu, tumeshuhudia makosa yakifanywa na waamuzi ama ya kibinadamu ama maksudi.

Mfano makosa ya kutoa penalty yamekuwa yakilalamikiwa sana. Hata hivyo yanaweza kuonekana ni makosa ya kibinadamu na hasa ukizingatia kuwa hata kwa wenzetu walilazimika kuwa na VAR.

Ila kuna yale ya timu kunyimwa penalty za wazi kabisa kwa kuogopa kelele za washabiki. Au unashangaa kipa kadaka mpira akiwa golini ila mwamuzi anasema ni kona! Vitu hivi vinafanya waamuzi wasiaminike kabisa.

Hawa utopolo wamefaidika sana na waamuzi na sasa hizi mbinu zao za kulalamika zinawafanya waamuzi wachezeshe kwa hofu.

Juzi nilimsikia mhamasishaji wa uto akisema Zanzibar Simba watakwama kwa sababu waamuzi wanatoka msikitini kwenda kuchezesha. Sasa ninashangaa kwani ukiangalia hata ushindi wa uto ana point 4 tu, wakati Simba wameshinda mechi zao mbili tena kwa magoli mengi.

CAF champions League Simba walishinda Nigeria.Wameshinda nyumbani.Je ni waamuzi wanaoifanya ishinde?

Utopolo acheni kulalamika kama mama mwenye mimba ya teja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…