Yanga wameamua kuhamishia hasira zao FCC?

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Hii nchi ni ngumu sana. Unaweza kumpa mtu elimu ukatarajia ataacha tabia zake za wanga, ila akisoma anaanzisha aina mpya ya wanga.

Niseme wazi kuwa, hao utopolo, baada ya kushindwa kwenye pitch, wameamua kupeleka hasira zao FCC. Baada ya wao kuisaidia Simba kudai bilioni 20, na kuona hakuna anayewajali, sasa kwa kutumia watu wao wameamua kupitia FCC ili kuiyumbisha Simba, hasa muda huu wanapoiona inapasua kimataifa.

Lengo lao ni kutaka wachezaji wakubwa waingiwe hofu kusaini Simba kwa kuwaaminisha eti kuna figisu.

Sisi Simba tuko imara. Njooni kwa akili. Michezo hiyo mkiiendekeza mjue inarudisha nyuma maendeleo ya soka
 
Kwani hizo bilioni 20 zinatakiwa kuwekwa kwenye klabu kama ahadi ya mwekezaji inavyo takiwa kutekelezwa, au wanalipwa hao utopolo?

Na hao utopolo unao wataja hapa, wanahusika vipi na hilo sekeseke la mwekezaji wenu mbambaishaji na hao FCC?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…