Yanga wamshukuru sana Haji manara

Yanga wamshukuru sana Haji manara

Do santos

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2011
Posts
635
Reaction score
338
Kwa Uongozi, washabiki na wanachama wa klabu ya Yanga hawanabudi kumshukuru sana Msemaji wa timu ya Simba Haji Manara kwa kuitumia vizuri nafasi yake ya usemaji wa Simba kwa kuitangaza zaidi Yanga.

Nimekuwa nikimfuatilia Haji kwa muda sasa aidha kwenye Mikutano na waandishi wa habari au kupitia Ukurasa wake wa Instagram.

Ni nadra sana kutokuitaja timu ya Yanga iwe kwa wazi au kwa njia ya mafumbo.

Kuna mifano mingi ya haya nisemayo. Lakini angalia tukio la hivi karibuni. Jinsi alivyoipa Promo wiki ya Mwanachi (Tamasha la Yanga) kwa namna kubwa kiasi cha kufanya iwe gumzo kubwa katika nchi.

Sio kwamba Yanga hawakuwa wanatangaza la hasha. Haji pia amehusika kutangaza kwa namna ya utani lakini ujumbe ulikuwa unafika kwamba kuna Wiki ya Mwananchi.

Timu ya yanga iliweka kambi Morogoro, lakini muda mrefu Haji amekuwa akiizungumzia kambi hiyo kwa dhihaka, lakini amesaidia sana kuonesha picha za wachezaji wakiwa kwenye kambi hiyo ya Morogoro.

Kwa shabiki wa Yanga kupitia Page ya Haji aliweza kupata taarifa za maendeleo ya klabu hiyo huko Morogoro. Yanga wamshukuru sana Haji.

Angalia hili la juzi, alipoweka kabisa Post ya Tangazo la mkutano wa yanga na waandishi wa habari. Pamoja na post hiyo, Caption haikuwa na maana yoyote zaidi ya kutoa taarifa ya mkutano wa Yanga na waandishi. Eti kwa sababu wanafanyia Serena Hotel? Ndio utani? Au Promo?

Kwa wachunguzi wa mambo, ni kama mtu aliyevaa uhusika fulani lakini moyo na mapenzi yapo kwengine. Ni kama mshahara unalipwa na huyu lakini kazi unamfanyie Yule.

Kuna wanaoona anatania. Yaani Yanga ni watani zake. Sawa.

Lakini umejiuliza katika utani huo. Kuna ulazima wa kutuma Post yenye tangazo la mkutano wa waandishi?

Ukurasa anaotumia ni wake na yeye ndio mwenye mamlaka nao na hapangiwi cha kutuma inaweza kuwa hoja ya wengine. Lakini ni sawa kuwazungumzia sana wapinzani wa muajiri wake.

Kuwapa nafasi kila siku kwa hili au lile? Ni sawa kuwazungumzia wapinzani kila kukicha kuliko waajiri wako?

Upo tayari mkeo awe anamzungumzia X-wake kila kukicha chumbani kwako japo iwe kwa ubaya?
Akwambie baby wewe unajua kuliko X wangu wa zamani. Iwe kila siku. Unadhani utaona ni sawa?

Nawashauri wana Yanga waache kumzodoa Haji manara kwani anawafanyia kazi kubwa kuliko wanavofikiria. Tena bila ya malipo.
manRA.JPG
 
Sema jamaa yupo tu simba kimasilahi lakin yeye ni yanga damu

Acha awapige hawa mambumbumbu siku wakishituka ashachuma vya kutosha
 
Tena aliposema Yanga ikijaza uwanja anaacha kazi Simba ,mashabiki Wa Yanga watajaa Sana ,usikute kweli anatumwa na Yanga
 
Utani wa yanga na simba hiwa naupenda sana aisee

Hahaha dah na hivi sa hivi simba wana mipesa

Wananchi huku wanasumbuka

Kuna kipindi wananchi nao watapata mipesa simba watafulia goli linahama

Maisha ya hawa watani ni raha sana [emoji28]
 
Sawa msemaji wa simba tumekusikia 😁😁 ametoka kiranga kujisifia kupitia ID fake ya Balaka, na Gentamice kupitia ID moja ivi nimeisahau. Leo Manara kupitia ID mpya. Karibu sana Manara karibu sana 😁😁
 
Yanga imshukuru mzungu pori. Pori lenyewe la michongoma.
 
Huna lolote mzembe wewe mkia fc, yanga huijui au,ndo inaongoza kwa mashabiki lukuki. Hakuna cha haji wala anakuja
Kwa Uongozi, washabiki na wanachama wa klabu ya Yanga hawanabudi kumshukuru sana Msemaji wa timu ya Simba Haji Manara kwa kuitumia vizuri nafasi yake ya usemaji wa Simba kwa kuitangaza zaidi Yanga.

Nimekuwa nikimfuatilia Haji kwa muda sasa aidha kwenye Mikutano na waandishi wa habari au kupitia Ukurasa wake wa Instagram.

Ni nadra sana kutokuitaja timu ya Yanga iwe kwa wazi au kwa njia ya mafumbo.

Kuna mifano mingi ya haya nisemayo. Lakini angalia tukio la hivi karibuni. Jinsi alivyoipa Promo wiki ya Mwanachi (Tamasha la Yanga) kwa namna kubwa kiasi cha kufanya iwe gumzo kubwa katika nchi.

Sio kwamba Yanga hawakuwa wanatangaza la hasha. Haji pia amehusika kutangaza kwa namna ya utani lakini ujumbe ulikuwa unafika kwamba kuna Wiki ya Mwananchi.

Timu ya yanga iliweka kambi Morogoro, lakini muda mrefu Haji amekuwa akiizungumzia kambi hiyo kwa dhihaka, lakini amesaidia sana kuonesha picha za wachezaji wakiwa kwenye kambi hiyo ya Morogoro.

Kwa shabiki wa Yanga kupitia Page ya Haji aliweza kupata taarifa za maendeleo ya klabu hiyo huko Morogoro. Yanga wamshukuru sana Haji.

Angalia hili la juzi, alipoweka kabisa Post ya Tangazo la mkutano wa yanga na waandishi wa habari. Pamoja na post hiyo, Caption haikuwa na maana yoyote zaidi ya kutoa taarifa ya mkutano wa Yanga na waandishi. Eti kwa sababu wanafanyia Serena Hotel? Ndio utani? Au Promo?

Kwa wachunguzi wa mambo, ni kama mtu aliyevaa uhusika fulani lakini moyo na mapenzi yapo kwengine. Ni kama mshahara unalipwa na huyu lakini kazi unamfanyie Yule.

Kuna wanaoona anatania. Yaani Yanga ni watani zake. Sawa.

Lakini umejiuliza katika utani huo. Kuna ulazima wa kutuma Post yenye tangazo la mkutano wa waandishi?

Ukurasa anaotumia ni wake na yeye ndio mwenye mamlaka nao na hapangiwi cha kutuma inaweza kuwa hoja ya wengine. Lakini ni sawa kuwazungumzia sana wapinzani wa muajiri wake.

Kuwapa nafasi kila siku kwa hili au lile? Ni sawa kuwazungumzia wapinzani kila kukicha kuliko waajiri wako?

Upo tayari mkeo awe anamzungumzia X-wake kila kukicha chumbani kwako japo iwe kwa ubaya?
Akwambie baby wewe unajua kuliko X wangu wa zamani. Iwe kila siku. Unadhani utaona ni sawa?

Nawashauri wana Yanga waache kumzodoa Haji manara kwani anawafanyia kazi kubwa kuliko wanavofikiria. Tena bila ya malipo.
View attachment 1171044
 
Back
Top Bottom