Yanga wamteua Dissmas Ten kuwa msemaji, Jerry Muro atupiwa virago

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
KATIBU Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa leo amemtambulisha Dissmas Ten kuwa Ofisa wa Habari wa nne wa klabu hiyo tangu mwaka 2010, akichukua nafasi ya Jerry Muro anayeondoka baada ya kumaliza mkataba wake.

Louis Sendeu alikuwa Ofisa Habari wa kwanza wa Yanga mwaka 2010 chini ya Mwenyekiti, Wakili Imani Mahugila Madega na akaendelea na kazi hadi chini ya Mwenyekiti Wakili Lloyd Baharagu Nchunga kabla ya kuondolewa kufuatia kuingia madarakani kwa Mwenyekiti Yussuf Manji.

Baraka Kizuguto akakaimu kwa muda nafasi hiyo, kabla ya naye kuondolewa na kuingia Muro ambaye hata kabla ya kumaliza mkataba wake, alifungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa makosa ya kimaadili.

Na siku chache baada ya kumaliza adhabu yake, Muro anaondolewa kazini na nafasi yake ikichukuliwa na Ten, aliyekuwa Ofisa Habari wa klabuya Mbeya City ya Mbeya.
Katika mkutano na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Ten ameahidi kuleta mapinduzi katika Idara ya Mahusiano na Mawasiliano ya Yanga.

Amesema anataka kuifanya Idara hiyo iwe moja ya vyanzo vya mapato vya klabu kupitia akaunti zake mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Na Mkwasa akasema Ten atafanaya kazi na Godlisten Anderson ‘Chicharito’, ambaye alikuwa anafanya shughuli za Idara hiyo kipindi chote cha mwaka mmoja uliopita kufuatia kufungiwa kwa Jerry Muro.

 
Katibu Mkuu wa Yanga SC, Boniface Mkwasa amemtangaza Dismas Ten kuwa msemaji rasmi wa club hiyo, Dismas anachukua nafasi ya Jerry Muro.

 
Muro hajaondolewa bali mkatabata umeisha. Tafuta lugha isiyo na ukakasi. Mfano, Mkataba wa Jerry Muro umemalizika n.k

Sent from my TECNO M3 using JamiiForums mobile app
 
Muro hajaondolewa bali mkatabata umeisha. Tafuta lugha isiyo na ukakasi. Mfano, Mkataba wa Jerry Muro umemalizika n.k

Sent from my TECNO M3 using JamiiForums mobile app
Anzisha uzi wako....!
 
POA. punguza povu

Sent from my TECNO M3 using JamiiForums mobile app
 
Huyu Dismas Ten simfahamu vizuri lakini kupitia taarifa mbalimbali na mahojiano ambayo amekuwa akifanya na vyombo vya habari anaonekana kama ni true professional. Klabu kubwa kama hizi lazima ziwe na wasemaji wanaojua kuutumia mdomo kwa mawasiliano ya umma na kujitofautisha na taarifa za kwenye vijiwe vyetu vya kubishana
 
Huyu Muro kuna kitu alikanyaga sio bure

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…