Yanga wanaandaa Event kuwacheka waliokufa kishujaa

Madumbikaya

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2018
Posts
639
Reaction score
1,919
Timu ya Young African wameandaa event itakayofanyika ukumbi wa JNICC (Julius nyerere ) kwa lengo la kufundisha mashabiki wao jinsi ya kufurahi na kuwacheka waliokufa kishujaa

Yanga wanaamini hakuna kufa kishujaa bali kufa ni kufa tu.

Event hiyo itakuwa kwa muundo wa kisasa lakini lengo kuu ni kufundisha mashabiki jinsi ya kufurahi na kuwacheka waliokufa kishujaa.

Yote haya ni maandalizi ya kufurahia nusu fainali ya CAFCC.

Taaluma hiyo kwa mujibu wa msemaji ni muhimu kwa mashabiki wake na mpango umeanza kutekelezwa siku ya robo fainali kwa kuimba nyimbo mpya kama "Hatuna jirani Sie".

Vionjo vya wimbo"Hatuna jirani sie"ni kejeli tosha kwa waliokufa kishujaa kwani umejaa maudhi,karaha na kusononesha.

Chanzo ni Azam media
 
Yani jirani yangu toka amepoteza kazi amekuwa mtu wa makasiriko.

Nikipiga bia zangu anasema namringishia yeye kisa hana ela ya kupiga bia. Nikifanya tafrija analalamika kuwa nafurahia yeye kufukuzwa kazi.

Jamani kila mtu apambane na life lake ukifail wewe hainifanyi mimi nishiriki kwenye majonzi yako.
 
Furahini sana.....ndio wakati wenu huu.
 
Viongozi wa Yanga wasikubali mafanikio mazuri yaliyo fikiwa yakatiwa doa na wajinga wachache. Nafikiri katika hatua hii Yanga inahitaji support ya kila Mtanzania
 
Viongozi wa Yanga wasikubali mafanikio mazuri yaliyo fikiwa yakatiwa doa na wajinga wachache. Nafikiri katika hatua hii Yanga inahitaji support ya kila Mtanzania
Na hawataamini pale wanaowacheka watakapochukua kombe kuanzia ligi kuu mpaka fa pamoja na kuongoza ligi msimu mzima
 
Benchi la ufundi linaumiza kichwa kwa ule utopolo waliocheza yanga jana walishindwa kuifunga team mbovu halafu mashabiki wanaleta ujinga kama huu kwa mpira gani mlio nao.
 
huu ni ujinga japo mie ni yanga
 
Benchi la ufundi linaumiza kichwa kwa ule utopolo waliocheza yanga jana walishindwa kuifunga team mbovu halafu mashabiki wanaleta ujinga kama huu kwa mpira gani mlio nao.
Lengo lilikuwa kufuvu.

Hakuna sababu ya kukamia mechi ili tuwachoshe wachezaji ikiwa tuna mechi ngumu za ligi na FA na Semi Finals ndani ya mwezi mmoja.

Ndio maana akaitwa PROF NABI.
 
Siku zote najuaga viongozi wa utopolo ni wapumbavu lakini sikuwahi kufikiria kuwa ni wapumbavu kwa kiwango hichi.

Sasa hiki ni nn aisee?
 
Sio wamekufa kishujaa, wamekufa Viume!
 
Vijana wengi wameanza kufuatilia mpira Baada ya
Betting, Instagram, nk

Wengi wao wanaujinga wa kutokujua historia ya Matukio ya Nyuma.

Simba imecheza Fainali 1993.
Kombe la washindi.

Ikacheza Nusu Fainali ya washindi Mwaka 1974.

UONGOZI WA SIMBA HAUJAWAHI KUANDAA EVENT YA KIPUMBAVU KAMA HIYO.

VIJANA TUKIAMINIWA TUFANYE MAMBO YA MAANA, HAMJIFUNZI HATA KWA MAKONDA, SABAYA.

TUMEWAPA WAJINGA WATUONGOZE.
 
.

Sent from my V2204 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…