MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Utulivu, Malengo na Focus za wachezaji wa Yanga ni wa hali ya juu sana. Kuna namna naona hii timu safari hii haijadhamiria sana taji la Ligi (japo hii inatokea tu automatically kutokana na ubora alio nao) Ila malengo hasa ni katika Ligi ya mabingwa barani Afrika.
Hii inathibitishwa na aina ya matokeo ya Yanga mpaka sasa, michezo 8, haijaruhusu goli hata 1, imeshinda michezo yote! huu ni ubora wa viwango vya juu mno!
Timu kubwa duniani pekee ndizo zinazoweza kufanya hivi, Hii ina maana hakuna club yenye ubora unaokaribia Yanga Tanzania, kuilinganisha Yanga na vilabu vya Tanzania kama kengold, coastal union,simba sijui JKT ni sawa na John cena yule wa miaka ya 2010 apande ulingoni na mwasibu!
Kilichobaki kwa Yanga sasa ni kuudhihirisha ukubwa wao Afrika, ambapo pia itakuwa ni suala la muda kuchukua mataji ya Afrika.