Yanga wanastahili pongezi za dhati

BETONY

Senior Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
188
Reaction score
170
Kwanza niwasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kazi iendelee

Ili mchezo wowote uendelee na kuwa sawa kunakuwa na kanuni mama za kuongoza mchezo huo, kwa manufaa ya wasimamizi na washiriki.

Jana ilikuwa siku adhimu katika soka la Afrika, kwani kariakoo Derby ni moja kati ya Derby 7 bora za Afrika. Nchi usimama kwa dk tisini na kugawanyika vipande viwili sawa kijani na njano na nyekundi na nyeupe.

Maandalizi ya mchezo huo ni zaidi ya dk 90 uwanjani. Mtakubaliana nami kuwa wote tunapenda mpira wetu uendeshwe kiuweledi. Sayansi ya mpira inaenda mpaka kwenye mda wa kula kwa wachezaji, mapumziko baada ya kula, mda wa kuwasirii uwanjani, maandalizi ya upashaji mwili moto na mda wa kuanza mchezo. Na siku ya mechi kubwa, ratiba ya vitu hivyo vyote utegemea mda wa mchezo. Kwa mfano mda wa wachezaji, kula, kunywa na kupumzika utegemee mda wa kuanza mchezo. Kiutaratibu hauwezi kusogeza mda mbele zikiwa zimepaki saa tatu, wakati timu zikija uwanjani.

Ni kweli kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kutokea na kusogeza mda wa kuanza mchezo, kukiwa na sababu kama hizo, pande zote nne mpaka tano (Wenye mpira wao TFF, Serikali, Simba, Yanga na Mdhamini au mrusha matangazo ya video) wanatakiwa kwa pamoja ndio watoe tamko la kwanini mchezo utapelekwa mbele. Hii itapelekea kuwa na maamuzi jumuhishi.

Haitakiwi kuwa kama ilivyoyokea jana kwa klabu kupewa taarifa sijui kwa barua au kupigiwa simu mda mfupi huku zikiwa njiani kuja kwenye mchezo. Ambacho kingetakiwa ni kwa bodi ya ligi, huku ikiwa pamoja na wawakirishi wa vilabu kutokea kwa pamoja na kueleza uhairisho huo.

TFF katika hili wanatakiwa kuomba radhi na kuwajibishwa, kwani wao ndio baba wa mpira na wanatakiwa kujua kanuni na taratibu. Serikali kupitia Waziri wa Michezo pia inatakiwa kuja na majibu kwanini ilitoa maelekezo ambayo hayakuwa jumuhishi kwa wote. Ni kweli kuna mambo ambayo labda Serikali iliona mchezo huo ni muhimu kupelekwa mbele, lakini wangezishirikisha pande zote kufikia ujumla wa pamoja.

Kwa kuzingatia kanuni na sheria za mpira Yanga wako na haki ya kufanya yale waliyoyafanya. Pia tukumbuke makosa ya nyuma, hayapelekea utaratibu wa makosa kuw sehemu ya kila siku.

TFF mmevuliwa nguo, uungwana ni kuchutama na kujisitiri, lakini lazima sakata hili liondoke na baadhi ya watu ili iwe fundisho na kutoa ujumbe kuwa, hatutakubali mpira kuchezewa.
 
Kwa nini mechi dhidi ya Azamu hawakuigomea?
Je mechi na Azam, klabu hazikushirikishwa kwenye maamuzi? Taarifa ya kusogezwa kwa mda wa mchezo kati ya Yanga na Azam ilitolewa siku 2 kabla ya mchezo na kanuni zilikuwa zinaruhusu. Pia Yanga kama timu mwenyeji siku hiyo waliwashirikisha Azam katika maamuzi ya pamoja
 
Sio kweli, mechi ya Azam na Yanga muda umechenjiwa ndani ya 24 hrs hata primechi meeting ishafanyika.
 
Sio kweli, mechi ya Azam na Yanga muda umechenjiwa ndani ya 24 hrs hata primechi meeting ishafanyika.
Tunabishana nini wakati kwenye account ya Yanga taarifa iliwekwa siku mbili kabla ya mechi. Nenda kaamgalie
 
Sio kweli, mechi ya Azam na Yanga muda umechenjiwa ndani ya 24 hrs hata primechi meeting ishafanyika.
Angalia hapo taarifa rasmi ya mda wa mchezo wa Azam na Yanga. Tusiende na mihemko
 
Kupitia hili sakata nazani ni wakati sahihi kwa mzee wetu, Mzee Mwinyi aje kufuta hadharani kauli yake ya Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu maana Mabingwa wa Nchi Yanga wameonesha kujitambua na kuondokana na uzwa wa TFF
 
Ukweli ni kwamba uoga ulipelekea kupata sababu ya kugomea mechi kama wangekuwa wanacheza na timu nyingine wasingegoma
 
Ukweli ni kwamba uoga ulipelekea kupata sababu ya kugomea mechi kama wangekuwa wanacheza na timu nyingine wasingegoma
Baki hivyo, katika kupigania yale wanayo amini walishapima sababu hizi kama zako. Lkn wakasema bora yawe hivyo hivyo tu. Yanga wanastahili pongezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…