Klabu ya Yanga imepigwa faini ya shilingi milioni 100 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kukiuka kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara katika mchezo namba 233 dhidi ya JKT Tanzania, uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-0.
Adhabu hiyo imetolewa baada ya wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi wa Yanga kushindwa kutumia chumba rasmi cha kuvalia katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam, na badala yake kutumia nyumba iliyopo nje ya uwanja upande wa pili wa barabara, kinyume na Kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.
Soma: Nashauri iundwe 'Yanga Law'; timu itakayokaidi kutumia 'Vyumba rasmi vya kubadilishia Nguo' ipokwe alama tatu na kutozwa faini ya Tsh. Milioni 50
Adhabu hiyo imetolewa chini ya Kanuni ya 27:7 ya Ligi Kuu kuhusu vyombo vya maamuzi. Sambamba na hilo, Kamati hiyo pia imewapeleka Rais wa Young Africans, Hersi Said, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Andre Mtine, kwenye Kamati ya Maadili ya TFF kwa ajili ya kutoa maelezo ya msingi kuhusu ukiukwaji huo unaodaiwa kujirudia.