Yanga Ya Lwandamina yachezea kichapo vs JKU

PROSPER 05

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
226
Reaction score
217
Ikicheza Soka la Ki-Barcelona Yanga imepoteza mechi yake ya kwanza chini ya Kocha George Lwandamina.

JKU ya Zanzibar ndiyo iliyoitia njaa Yanga kwa kuichapa mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Yanga ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi mapumziko ndipo Lwandamina akabadili kikosi chote kwa asilimia 95.Hata hivyo, bado hakuweza kuabdilisha lolote kwa kuwa hadi mwisho, JKU iliibuka na ushindi.
MABAO yote mawili yalifungwa na mshambuliaji, Emanuel Martin.

Mchezaji huyo wa zamani wa JKT Mlale, Martin alifunga bao la kwanza dakika ya 12 kwa shuti kali akiunganisha kona iliyopigwa na Mbarouk Chande wakati la pili alifunga dakika ya 27 akimalizia pasi ya Nassor Mattar.

Washabiki Wa..... KAMA Hawaamini Kilichokua kinaendelea
 
JKU sio mchezo. Angalia sura za migongo wazi. Zinatia huruma.
 
Kumbe ni mechi ya kirafiki, basi haina shida mbona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…