Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,904
- 1,064
Habari zilizopatikana toka Bukoba zinaeleza kwamba Yanga imeumizwa na Kagera Sukari goli 2 bila majibu.
Wakati huo huo habari zinaeleza kuwa nao Simba nao wamelia kwa Azam goli mbili hizo hizo.
Ama kweli ni mwaka wa shetani.
Afadhali maana angebamizwa mmoja kati ya Simba na Yanga mmoja angetamba sana
Nimeambiwa mchezo ulikuwa mkali kiasi kwamba kila timu imepata majeruhi wa red card mmoja mmoja.🙁
Habari zilizopatikana toka Bukoba zinaeleza kwamba Yanga imeumizwa na Kagera Sukari goli 2 bila majibu.
Wakati huo huo habari zinaeleza kuwa nao Simba nao wamelia kwa Azam goli mbili hizo hizo.
Ama kweli ni mwaka wa shetani.
Ha ha ha ha Pole wewe unaelekea ni wa Jangwani ndiyo maana umesema afadhali, mie mpira wa bongo umeshaniboa miaka nenda miaka rudi migogoro kila mwaka hasa Simba na Yanga na hii sana katika inachangia kushusha kiwango cha soka Tanzania. Timu yangu Arsenal karibu tuadhiriwe tena leo lakini dakika za majeruhi tulisawazisha.
Weekend njema.

Kulikuwa na michezo miwili, unazungumzia mchezo gupi?
Huu bado ni MWAKA WA MUNGU WETU na si Mwaka wa SHETANI.
Kubamizwa kwa Yanga na Simba hakubadilishi chochote katika mwaka; Tena maisha ya kawaida ya mwanadamu wa Kitanzania yanaweza yakawa mazuri kuliko yalivyokuwa kabla.
HATA SIMBA NA YANGA WAKISHUKA DARAJA hadi daraja la tatu hauwezi kuwa mwaka wa shetani, bali utaendelea kuwa mwaka wa Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi.
Yanga na Kagera sukari
Ah,Halafu wewe inaelekea ni SIMBA!maana the way ulivyoweka heading ya thread yako!mimi nilishtuka nikafikiri Simba wamepeta kumbe yale yale tu!Tuambie basi na mechi ya SIMBA VS Azam ilikuwaje?
Timu kongwe zinapofungwa na timu changa inaleta utamu japo inauma.afadhali aloanza kufungwa leo kuliko anayeendelea kufungwa.
Heshima kwako mkuu..ngoja niende nje ya mada...vipi kuhusu lile goli la Van Persie???,mbona naona kama linesman katubania vile
Marefa naona wana njama za kutufutia magoli yetu, kutunyima penalty tunapostahili au opponent kupewa penalty ya kiushkaji. Inabidi uongozi wa Arsenal uje juu kuhusu hili au marefa wataendelea kutuminya kila mechi. Yule SAF hakosi kulalamika kila siku kuhusu marefa hata kama wao ndiyo waliopendelewa, lakini Wenger huwa hatii neno.