Yanga yadaiwa Sh Bilioni 5

fungi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
2,539
Reaction score
4,672
TAARIFA ya mapato na matumizi ya klabu ya Yanga inaonyesha kwamba deni la klabu hiyo sasa limefikia Sh 5.4 Bilioni.

Taarifa hiyo kwa mwaka 2016 imeonyesha kuwa Yanga alikopa kiasi cha Sh 1.5 Bilioni kwa msimu wa 2015/16 ili kuziba pengo lilijitokeza katika bajeti yao kitendo ambacho kimefanya deni hilo lifikie Sh 5.4 Bilioni.

“Kwa miezi 12 tumekuwa na Sh 1.5 Bilioni ambayo klabu imekopa bila riba, na imekuwa ikikopa kwa miaka kadhaa na imeshindwa kulipa,” ilisomeka taarifa hiyo. “Mkopo unatoka kwa mwanachama mmoja wa timu ambaye hadi sasa kachangia Sh 1.5 Bilioni na kwa miaka 10 mkopo umefikia Sh 5.4 Bilioni,’’ilieleza taarifa hiyo.

Pia imebainika kuwa kwa mwezi huu (Agosti) Yanga itahitaji Sh 500 Milioni kuendesha shughuli zake mbalimbali, ukiacha Sh 88 milioni zinazotokana na udhamini wa Kampuni ya Quality Group.

Licha ya taarifa hiyo kutomtaja mwanachama anayeidai Yanga, Mwanaspoti inafahamu kuwa ni Quality Group ndiyo inayotoa mkopo huo kwa udhamini wake na imekuwa ikifanya hivyo miaka 10 sasa.

Kutokana na kutokuwepo kwa mapato ya kueleweka Yanga, deni hilo linatarajiwa kuendelea kukua katika miaka miwili ijayo kwani mpaka sasa hakuna marejesho yoyote aliyoanza kufanyika.

Katika mkutano mkuu wa dharura hivi karibuni, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi Quality Group kabla ya kujitoa aliwataka wanachama wa Yanga kubadili mfumo wa uendeshaji ili wamkodishie timu na nembo aiendeshe kwa faida na kuwapa mgao wa asilimia 25.
 
He he heee! Jamaa ameanza kudai hela alizokuwa anatoa kama msaada. Hapo kwa kuiweka bajeti hadharani jamaa ametegesha kwa atakayejipendekeza kuichukua timu akute deni na alazimike kulilipa, kwa hiyo ni kama vile anawatishia wana Yanga kwamba wasithubutu kumleta mtu mwingine zaidi ya yeye, ila wakimleta basi akubali kulipa 5B
 
Hivi hizo timu zetu zinaendeshwaje?

Ni kikao gani kinapitisha bajeti ya timu ya kila mwaka?
Ni kikao gani kina mamlaka ya kuruhusu timu kukopa na kwa kiwango kipi?
G
Je, mahesabu yakishakaguliwa na "mkaguzi wa nje" wanachama HUPATA wasaa wa kujadili?
 
Ndio matatizo ya timu kumilikiwa na wanachama,haina hata vyanzo vya mapato.
 
kumbe ndio maana anataka aikodishe timu bureee!,nilitaka kushangaa,yaani timu inakodishwa kama fremu za duka!
 
Afu utasikia Wana yanga wakisema yanga ina hela kweli! Kumbe wanasahau kuwa ni Za mtu binafsi
 
Kujidai kote kumbe wamekopa? Mabwaku ati Wakimataifa Tunauza Basi sisi ni watu wa Kupanda Ndage tu ndio tunataka kununua Ndege yetu... BAflesho wanajidai babukubwa kumbe wanadaiwa... Soon tutasikia wakitembeza mkopo kwa waendesha boda boda
 
Wananchi wa Mbagala walisema wametapeliwa na Manji na kuionya Yanga sasa wataamini... Salender the Team ni Mr. India

Eh Mugambo Kushual
 
Wajinga ndio wanaotafunwa.
Kama miaka yote anajikopesha halafu hakuna hela inayorudi na bado watu mna imani naye kisa kaifunga simba mara mbili.
 
Mbwembwe nyingiii,kumbe madeni kibao...hawa kambale shida sana..
 
Hahahahaha! Timu zote za Tanzania zinatakiwa ziwe chini ya kampuni au chini taasisi fulani itakayoendeshwa na management kabisa, hii ya kuongozwa na wanachama ni hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…