Yanga yajiharibia yenyewe kwa kuingiza siasa kwenye SIKU YA MWANANCHI

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mchezo wa soka ni miongoni mwa michezo inayokusanya watu wa itikadi tofauti kabisa , mnaweza kuwa na makandokando yenu ya kisiasa lakini mkaja kukutana kwenye soka , kwa kifupi soka ni ya Wanamichezo .

Kitendo cha Yanga kumtangaza Mzee Kinana ambaye ni Kiongozi wa Juu wa CCM Kuwa mgeni rasmi wa siku yao waliyoipachika jina la SIKU YA WANANCHI , si tu kwamba hakikubaliki , Bali kinaleta sintofahamu kwa wale wana yanga ambao si wanaccm .

Mbona viongozi wa serikali ni wengi tu , kwanini aalikwe kiongozi wa ccm , Waalikaji wamelenga nini ?
 
Mchezo wa soka ni miongoni mwa michezo inayokusanya watu wa itikadi tofauti kabisa , mnaweza kuwa na makandokando yenu ya kisiasa lakini mkaja kukutana kwenye soka , kwa kifupi soka ni ya Wanamichezo .
mbona hoja yako inaji contradict yenyewe!

kinana yuko pale, kwa uyanga wake na si kwa uccm wake.
 
Usiifananishe yanga na vitu vya kijinga aiseee.....mbona koloz nyie mnae jobo aliyekua spika wa jengo inapokaa siwa bila kumsahau kiranja wa mawaziri wote..wote wapo kwenu koloz.
 
Sisi matrafiki tumemaindi sanaa, huyo kuwa mgen rasmi wametuboa snaa
 
Hizi team za Kariakoo zote zinafanana,hamna wa kumcheka mwenzake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…