Yanga yakabidhiwa Kiwanja

Jackson94

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2016
Posts
492
Reaction score
560


Klabu ya Mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imefunguka na kudai wamekabidhiwa kiwanja chenye takribani hekari 50 Mkoa Dodoma kwa lengo la ujenzi wa 'academy' itakayokuwa inakuza vipaji vya vijana wadogo nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na uongozi huo kupitia ukurasa wao maalum wa kijamii asubuhi ya baada ya kumaliza shughuli za ufunguzi wa tawi la jipya la Yanga katika makao makuu ya nchi, mkoani Dodoma.

"Wanachama wa Yanga tawi la Dodoma Makao Makuu kupitia mlezi, Naibu waziri wa kazi, vijana na Ajira , Antony Mavunde, wametoa eneo la hekari 50 kwa Yanga SC kwa ajili ya ujenzi wa 'academy' ya klabu itakayokuwa na jukumu la kutafuta, kukuza na kendeleza vipaji kwa vijana wadogo ili waje kuwa wachezaji wakubwa wa Yanga katika siku za usoni", imesema taarifa hiyo.

Kwa upande mwingine, matumaini ya Yanga SC kutetea ubingwa wake wa Ligi kuu Tanzania Bara yamezidi kuonekana kuwa hafifu baada ya jana Aprili 22, 2018 kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Mbeya City uwanja wa Sokoine na kusababisha kuwa na alama 48 katika mechi 23 huku wakiwa wamezidiwa alama 11 na watani wao wa jadi Simba SC wenye pointi 59 za mechi 25 na wababe hao watakutana Jumapili uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Bora Muhamie huko, mjini hampawezi, kila mwaka mnakumbwa na mafuriko.
 
Msianze kufyeka na mashoka kama walivyofanya wenzenu kwenye kiwanja chao cha Bunju
 
Yanga bhana si walipewa Kiwanja na manji sijui eka 600 huko Kigamboni!?ziliishia wapi!?
 
Million 600 imeshapangiwa matumizi tayari. Ila watani uwezo wa kifedha mnao au tamaa tu?
 
Yani Wameshindwa na Mshahara Wa [HASHTAG]#LuandaAmina[/HASHTAG] Akawatoka Nduki! halafu Wanataka Aajenge Academy utadhani wataijenga Kwa Maboksi πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Yanga bhana si walipewa Kiwanja na manji sijui eka 600 huko Kigamboni!?ziliishia wapi!?
Mwenyw nilishangaa sana kusikia wanaweka kifusi katikt ya bwawa wakt wana hekari 700 kigamboni.
Au zile zilikua kiininacho tu ili maji apewe uwekezaji ndani ya Yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…