Yanga yamsaini striker hatari wa Zanaco, Mosses Phiri

Anigrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
1,680
Reaction score
4,204
TETESI...! Inajulikana kuwa Simba walivutiwa sana na huduma ya huyu mchezaji mzambia kutoka katika club ya Zanaco, katika kipindi cha dirisha kubwa ila ikashindikana kutokana na idadi ya wachezaji kutimia

Wakajipanga kurudi tena katika dirisha hili dogo ila bahati mbaya Zanaco imefuzu hatua ya makundi shirikisho hivo kufuta matumaini ya Simba kumnunua phiri maana endapo kama watamnunua itabidi asitumike katika mashindano ya Shirikisho kama Sheria inavosema, Simba inataka kununua wachezaji wa kigeni Kwa ajili ya kuongeza nguvu Katika shirikisho

Inadaiwa kuwa Yanga ishamalizana na striker na kilichobaki ni kumalizana na uongozi wa club ya Zanaco na wamefkia hatua nzuri Kwa hiyo ni Jambo la muda tu Kwa Yanga kukamilisha usijili wa Mosses phiri

Kwa Yanga kumpata mchezaji huyu sio siri kwangu Mimi sasa rasmi nawaweka katika mbio za ubingwa maana wanaonekana wako serious na wamedhamiria Kweli msimu huu, jamaa ni fundi haswa ambae anaweza kucheza kama namba 9,10 lakini pia winger, Kwa ile striking force yao na kumuongeza huyu mwamba hapo sasa wamekamilika haswaaa
 
Watafute beki mbadala wa MWAMNYETO pale nyuma, huku mbele nafasi ya MOLOKO, na NTIBAZONKIZA zitafutiwe washindani halisi. Sina shia na katikati. Mbele pale tunahitaji mijitu inapiga MIWA hata akiwa karibu na kati.
 
Nimeona mahali kama vile Wasafi TV wamethibitisha usiku huu?
 
Watafute beki mbadala wa MWAMNYETO pale nyuma, huku mbele nafasi ya MOLOKO, na NTIBAZONKIZA zitafutiwe washindani halisi. Sina shia na katikati. Mbele pale tunahitaji mijitu inapiga MIWA hata akiwa karibu na kati.
Yaah Centre back muhimu sana Coz mimi sina imani sana yule kijana Ninja
 
Watafute beki mbadala wa MWAMNYETO pale nyuma, huku mbele nafasi ya MOLOKO, na NTIBAZONKIZA zitafutiwe washindani halisi. Sina shia na katikati. Mbele pale tunahitaji mijitu inapiga MIWA hata akiwa karibu na kati.
Moloko na tibazokiza wana shida gani?
 
Watafute beki mbadala wa MWAMNYETO pale nyuma, huku mbele nafasi ya MOLOKO, na NTIBAZONKIZA zitafutiwe washindani halisi. Sina shia na katikati. Mbele pale tunahitaji mijitu inapiga MIWA hata akiwa karibu na kati.
Kwa nafasi ya Moloko na Ntibazonkiza yupo Nkane na Ambundo na hata Ngushi ana uwezo wa kucheza akitokea pembeni,hapo kwa Mwamnyeto kweli ni muhimu apate beki mwingine mkali wa kumpa ushindani!
 
Kama ni kweli basi niwape hongera viongozi wa Yanga kwani wanathibitisha ni kwa kiasi gani wamepania kuipaisha timu yao kitaifa na kimataifa. Moses Phiri ni mtu hasa na Yanga pale mbele itakuwa moto kutakuwa hakuna timu ya kuisimamisha kwenye ligi yetu.
 
Na uyahifadhi haswa,tukutane mwisho wa msimu.Sote tunajua kilio kinachowajia mbele ya safari
Maisha yanabadilika mtani, Hali ya miaka iliyopita haiwezi kuwa sawa na hali ya mwaka huu na miaka ijayo

Tulikuwa tunaongoza Ligi tukiwa na kina Sarpong, Lamine Moro na vilaza wengine huku mildified akitegemewa Zawadi Mauya huku winga akiwa Kaseke na kina Nchimbi

Toka usingizini haraka sana, usije ukaanza kutoa kinyesi kwenye hiyo ndoto yako mtani
 
Mosses Phiri
Crispin Ngushi
Denis Nkane

Naomba kuhifadhi maneno yangu, Nisije nikamkufuru Mungu
Usiwe na hofu bro,kwanza ujue kuwa yacooba,atachelewa sana kurudi uwanjani,fei toto tunamuuza mwakani,deus kaseke tunamuuza geita gold,na kwa taarifa yako nabi anataka kila position iwe na wachezaji 3

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Wachezaji watatu kwa kila namba ni wengi sana, ndio maana baadhi ya wachezaji wanapaswa kuwa kuwa versatile ili wacheze namba zaidi ya moja. Kati ya eneo Yanga wanapaswa kulifanyia kazi ni pamoja na kutafuta kocha anayeeleweka. Uchezaji wa Nabi uko very predictable, pasi nyingi na mchezo wa taratibu ambao hauko aggressive hata kidogo.
Kwa wachezaji waliopo Yanga kwa sasa, hatupaswi kuwa na kuzuizi cha kubeba kombe la ligi au kuvuka hatua ya makundi club bingwa Afrika.
 

Kuna chizi akiona umesema kila nafasi iwe na wachezaji 3 atapiga hesabu ya 11 mara 3 itampatia 33 atauliza usajili mwisho ni wachezaji 30, hao 3 watasajiliwa.kwa taratibu zipi kumbe hajui kuna wachezaji wanacheza namba zaidi ya 1.
 
Hapo kwa Nabi umeongea utumbo m*v kabisa. Kuna kocha ambae kaleta taswira njema Yanga kuliko prof Nabbi?

Tunajua ww ni kolo unajificha kwenye kichaka cha Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…