Yanga yamsimamisha kazi mpiga picha wao

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Uongozi wa Yanga umemsimamisha kazi mpiga picha wao Chicharito,uongozi huo umemsimamisha huyo mpiga picha wao jioni ya leo baada ya kuingia kambini kupiga picha bila idhini ya uongozi.

Inasemekana uongozi ulikuwa na hofu kwamba ameangizwa na upande wa pili (watani wa jadi) kudadisi kinachoendelea kuelekea mechi ya kesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Yanga siyo kwa kweli. Hii Yanga siyo ile niliyoipenda enzi nipo mtoto nachukua karatasi naandika list yote ya Yanga kuanzia Rifat Said/Stephen Nemes mpaka Edibily Lunyamila. Hapo kati Sanifu Lazaro,Thomas kipese,Keneth Mkapa,Godwin Aswile,Salum Kabunda ,Issa Athumani,Athuman China,Said Mwamba na wengine kibao.
 
Yanga ni Yanga siku zote.
Kesho mnyama anakatwa mkia.
 
Duh kumbe na wewe ni mhenga. Hiyo squard weka mbali na watoto, mikia walikuwa wanakufa siku WK moja kabla.
 
Bi dada hii Yanga ya mwaka gani?
 
Basi wewe hujakua kipindi cha Edibily Lunyamila. Pole maana enzi hizo pia Simba alikuwepo Nteze John Lungu.
Watu wengi nawaonaga wanamsifia huyo Lunyamila basi inaonesha jamaa anajua mpira kwelkwel dah! Kiukwel nimekosa vitu vingi ila Hawa wachezaji ninaowaona sasa hiv ni pasua kichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…