Yanga yamsimamisha Niyonzima kwa utovu wa nidhamu!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Uongozi wa klabu ya Yanga, umetangaza kumsimamisha Haruna Niyonzima kwa muda usiojulikana.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amesema Niyonzima amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Amekuwa akifanya mambo ambayo yanaonyesha wazi ni ukiukaji mkataba hasa katika masuala ya utendaji.

Lakini amekuwa akionyesha utovu wa nidhamu. Kwani licha ya kukaa naye pamoja na kuzungumza naye kuhusiana na hali hiyo bado amerudia.

Tulikaa naye Novemba 4, ilikuwa pale Protea Hotel. Tukajadiliana na mwisho akaomba msamaha na kuahidi asingerudia tabia hiyo ya kuwa mchelewaji kurejea kazini kila anapokwenda Rwanda.

Lakini amerudia safari hii, tena akijua wazi alijiunga na timu ya taifa ya Rwanda bila taarifa kwa klabu. Halafu baada ya fainali ya Cecafa akazima simu kabisa, alisema Dk Tiboroha.
 

Attachments

  • NIYONZIMA+KAA.JPG
    36.1 KB · Views: 570

Professional wa East Africa ni sheeeeeeda na ulimbukeni tu. Akatiwe line hamna namna
 
Ndio maaana miafrika hatufiki mbali katika soka na mambo
mengine mengi tu, tumejaa ulimbukeni na majivuno .
kisoka namkubali sana huyo dogo Niyonzima ila kwa
huu ujinga alioufanya namchukia sana.
 
Aende kwa mikia inayo vumilia ujinga
 

kumbe Manji hakukosea pale aliposema sitaki tena wachezaji wa A. Mashariki.
 
Akae pembeni tu ninavyoijua yanga huyo ndiyo bas tena ataisikia tu yanga msimu ujao
 
Amevimba kichwa baada ya kuonekana ni mchezaji aliyependwa sana kwenye mashindano ya CECAFA.
 
Niyonzima ni jipu litumbuliwe tu na kiini kiputwe Kigali kabisaaa
 
Hizo ni sababu tu. Sababu kubwa ni kuna timu yanga wakicheza nayo jamaa anachezaga chini ya kiwango. Wamepata sababu ya kumsimamisha sasa
 
Hanamaana huyu aende kabisaa..
 
niyo amazingua sana siku hizi wampumzishe kwanza mzunguko wa kwanza uishe,yako majembe pale kati yatapambana tu.
 
Ataisikia bongo, aende mwenyewe mwadui
 
Sasa nafasi yake Jangwani haipo tena,,,,,,, mmemuona Kamusoko lakini?
Jamaa anatoa asist na kufunga pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…