Yanga yapanga kumrudisha Ngasa Jangwani ili wabebe Kombe la Shirikisho Africa!

Yanga yapanga kumrudisha Ngasa Jangwani ili wabebe Kombe la Shirikisho Africa!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Pamoja na uongozi wa Free State Stars ya Afrika Kusini kumzuia kiungo wake mshambuliaji, Mrisho Ngassa kumtoa kwa mkopo, nyota huyo amewatoa hofu mashabiki wa Yanga na kuwaambia siku si nyingi anarejea kwenye klabu hiyo.
Ngassa ameitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuwasili nchini kisha kutazama mechi ya fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga na Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo Yanga ilishinda mabao 3-1.
Ngassa alijiunga na Free State inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini, mwaka jana baada ya mkataba wake kumalizika Yanga.
Ngassa amesema viongozi wa Yanga ndio waliowafuata Free State kwa ajili ya kumuomba kwa mkopo ili aiongezee nguvu timu hiyo katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Ngassa alisema, bado mazungumzo yanaendelea kati ya pande hizo mbili kwa kushirikiana na yeye kuhakikisha anarejea Yanga.
“Nimefurahi sana kuonana na mashabiki wa Yanga na kunifurahia, wengi wao wameonekana kuwa na upendo na mimi waliponiona uwanjani, pia wakinihitaji nirejee kuiongezea nguvu timu hiyo kwenye michuano ya kimataifa.
“Hivyo niwatoe hofu tu kuwa mazungumzo yanaendelea vizuri kati ya Yanga na Free State timu inayonimiliki na Mungu akijalia, basi nitarejea kuichezea Yanga,” alisema Ngassa.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro alionekana kufichaficha mambo kwa kusema: “Hilo suala bado halijafika mezani kwangu, hivyo siwezi kulizungumzia. Ngassa bado ni mchezaji halali wa Free State, kwa hiyo mambo yakiwa tayari ndiyo naweza kulizungumzia
images-3.jpeg
images-7.jpeg
 
Utakuwa uamuzi mbovu sana kama Yanga watamrudisha Ngasa,timu sio level yake kabisa labda Simba au Stand United ndio kutamfaa
Naunga mkono hoja mkuu kwa sasa ngassa hana uwezo wa kufit yanga kwanza hata huko south ana mechi kibao hajaanza
 
Naunga mkono hoja mkuu kwa sasa ngassa hana uwezo wa kufit yanga kwanza hata huko south ana mechi kibao hajaanza
Kwani pengo la Ngassa limesha zibwa pale Yanga?

Ubora wa ligi ya kule kunafanya aonekane wa kawaida... Ila bado akija hapa ana uwezo wa kufanya vyrma zaidi ya Kaseke.
 
Mkuu hapana Kaseke ni habari nyingine kwani ni mchezaji anaepanda na kushuka kuja kumsaidia Oscar au Mwinyi,ngassa hana pumzi hiyo hata siku moja acha kupenda jina
 
Ngassa hapana, Yanga jipangeni kupata wachezaji watakaoisaidia timu kwa muda mrefu.
Msifanye kama wale watani wetu waliomsajili Mgosi kwa historia ya zamani. Haijalishi una mapenzi makubwa namna gani na club linapokuja suala la kuitumikia timu kama mchezaji, uwezo na umri wa mchezaji vinahusika sana.

Sikatai Ngassa ni mchezaji mzuri lakini kurudi Yanga kwa sasa hapana.
 
Ha ha ha h Bongo soka fitna sports club...tuna safari ndefu sana watanganyika..
 
Najiuliza tu Ngasa arudi Yanga kwa sasa kufanya nini.? Labda awe benchi la ufundi.!
 
Kwani pengo la Ngassa limesha zibwa pale Yanga?

Ubora wa ligi ya kule kunafanya aonekane wa kawaida... Ila bado akija hapa ana uwezo wa kufanya vyrma zaidi ya Kaseke.
Tangu aondoke pengo lake halijaonekana
Simon Msuva na Deus Kaseke wako vizuri sana kuliko Ngasa
 
Back
Top Bottom