Tango73
JF-Expert Member
- Dec 14, 2008
- 2,180
- 1,291
Timu isiyokuwa na academy ya kufundisha soka vijana uhai wake uko mashakani. Yanga punguza gharama za usajili nje na ndani ya nchi kwa kulea vijana wenye vipaji vya soka. Kusajili mchezaji kwa mabilion ya pesa toka nje ya nchi ambapo uchezaji wake hautishi kuliko wazawa ni kupoteza pesa tuu.
Mkoa wa Dar Es salaam una mamilion ya vijana wenye vipaji vya soka la kutisha isipokuwa hali ngumu ya maisha kutoka katika familia zao kuwagharimia kujiendeleza kisoka kunawadhoofisha sana vijana hao wafikiapo miaka 16! Hivyo matawi ya Yanga nje na ndani ya mkoa wa Dar yakifanya upekuzi wa vijana wenye vipaji kuja kujiendeleza kisoka clabuni itakuwa jambo la dhahabu sana.
Kama nchi hii imeweza kutoa wachezaji wakali kama Mogella, omari hussein,Pondamali, thueni Ally na Gaga hamisi basi accademic za watoto zitatoa wakali wa mfano wa messi na Neymar!
Nitafurahi sana kusikia kikosi cha Yanga kina wazawa wengi kuliko mamluki wakati timu ikiwa katika makundi ya CAF kuliko ilivyo sasa mbapo mamluki ni wengi timuni kuliko wazawa!hii itatimia ikiwa Yanga wakizingatia :ZIZI LISILO NA NDAMA SIKU ZOTE HALINA UHAI!