NEGLIGIBLE
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 354
- 92
Imekuwa ni kawaida kusikia watu wazima wakijiita yatima eti kisa ni kufiwa na wazazi..........Ninavyojua mimi msingi wa uyatima unaanza pale ambapo mtoto anapofiwa na mzazi/wazazi wakati akiwa chini ya malezi ya mzazi/wazazi.Hivyo kijana mwenye zaidi ya miaka 18 au 23 kama bado anasoma,hastahili kuitwa/kujiita yatima hata kama atafiwa na wazazi,vinginevyo kila mtu ni yatima.Kama niko sahihi kuna upotoshaji mkubwa sana wa neno yatima,watu wamekuwa wakilitumia kuhitaji huruma toka upande wa pili,kitu ambacho sio sawa............naomba nielimishwe kama siko sahihi,vinginevyo mamlaka zinazohusikua zielimishe watumia kiswahili juu ya matumimizi sahihi ya neno `yatima`