naona kuna watu wanaomba mungu atuepushie hili balaa, lakini ukiangalia kiundani ni kama tunakufuru mungu tu, wewe unaomba hili balaa lisitokee kwa kinywa chako, lakini kinywa hicho hicho kinalaani na kuwaombea wafe viongozi na wote wanaohusika kumnyima mwanano shule nzuri, wanaohusika kukunyima chakula kizuri cha rakaa tatu, wanaousika kukunyima matibabu stahili kwa wewe na familia yako, wanaohusika kukufanya ukakae mabondeni kusikokuwa na uhakika wa maisha hata ya masaa mawili yajayo, sijuhi mungu akusikilize wapi?
mungu alishatujalia neema kubwa sana katika hii nchi na ni kwa faida ya wote, lakini kuna watu wasiozidi laki tano ambao wanakula mali zote za watu karibu milioni 40.
Fujo uwaga zinakuja baada ya kukata tamaa na hakuna mtu anyekusikiliza wala kukusaidia na ndio mwisho inakuja ile roho ya bora nife, lakini nife kwa faida ya kizazi kijacho,
dalili zote za kutokea hii hali zipo,
"ni mawazo yangu tu mjomba"