Habari za jioni wakuu! Naamini wengi tushaanza kukubali kuwa JPM hatuko nae tena. Ni wazi kuwa maisha lazima yaendelee hivyo nimejikuta nawaza mustakabali wa taifa letu linakoelekea.
Kwanza kabisa wote tunajua kuwa JK ndo alimteua Mama Samia kuwa waziri 2010 -2015, lakini pia Ijumaa ya 26.3.2021 JK alisikika akisema yeye alihusika kuhakikisha Mama Samia anakuwa mgombea mwenza wa JPM 2015,
Pili ukifuatilia kwa ukaribu utagundua Mwinyi Jr na Samia wana ukaribu sana na hata baada ya kuapa kuwa rais Mama akimuita Mwinyi Jr kaka alimshukuru sana kwa ukaribu wake kipindi kile cha majonzi, wakati huo huo inaonekana Mwinyi Jr aliaminiwa na JK toka 2005 hadi 2015 kwa kumpa wizara mbalimbali ikiwemo wizara ya ulinzi na inasemekana alishaandaliwa kuchukua kijiti cha JPM kama yasingetokea yakutokea, hivyo tunaona kuwa JK=Mwinyi Jr=Samia.
Tatu ni kuibuka kwa kundi la Vigogo(2014 ,2021, Kigogo Kigogo nk) ambao siku zote wamekuwa wakimpinga JPM na team yake huku wakionekana kutoigusa na pengine kuisifia kwa mbali team JK (January, Nape, Ridhiwan, Membe, Nchimbi nk) kitu ambacho kimewaaminisha watu kuwa Vigogo ni team JK walio ndani na nje ya serikali ambao wanahisi kutengwa na JPM na sasa wanataka kurudisha nafasi zao . Vigogo wamekuwa wakipata taarifa hadi za Ikulu kabla hazijatolewa rasmi ikiwemo ya Kakoko kutumbuliwa ambayo wameitoa kabla ya Rais kusema hivyo inaonekana wamejikita kila sehemu na wameanza kuaminika kitu ambacho ni hatari sana pale wanapotoa taarifa zisizo sahihi kwa ajili ya maslahi yao..
Kwa muktadha huo, inaweza kuwa JK akalirudisha genge lake kwa kutumia ukaribu wake na Marais wote wawili? Mradi wa Bagamoyo na Gesi Mtwara inaweza kurudi kifisadi tena kwa kasi? Mikataba ya madini mibovu inaweza kurudi upya ? Makusanyo yanaweza rudi chini ya trioni moja ?
Sina imani kabisa na JK